Namna ya kukabili tatizo la upungufu wa nguvu za kiume-2



DK. STEPHEN KISAK

KAMA tulivyoona katika sehemu iliyopita kuwa picha, harufu au sauti huhusika kwa kiasi kikubwa katika kuamsha nguvu za kiume, pia tunaona lipo jambo jingine ambalo huhusika pia katika kuamsha nguvu za kiume.

Hisia: Katika eneo hili hisia kupitia katika mguso wa sehemu  ya mbele ya uume au hisia kupitia kuchochewa kwa mishipa ya fahamu kupitia kujaa kwa kibofu cha mkojo. Hali hizi mbili huamsha chocheo ambalo hupeleka taarifa haraka katika mishipa ya fahamu iliyopo katika uti wa mgongo na ghafla uamko hutokea.

Na hili limethibitishwa na watafiti wengi kwani ni mara nyingi wakati wa asubuhi uume huwa unakuwa umesimama kwa walio wengi na hata kwa watoto wadogo nyakati hizi za asubuhi na punde hukojoa.

Tatizo la kimwiliIli uweze kuwa na nguvu imara za kiume ni lazima uwe na mfumo mzuri wa mzunguko wa damu katika mwili wako, kama una matatizo ambayo hufanya mishipa ya damu kuwa midogo au magonjwa kama ya moyo, kiharusi, shinikizo la damu, ugonjwa wa kisukari na mataizo ya tezi la shingo.

Matatizo mengine mfano magonjwa ya mishipa ya fahamu, upasuaji kipindi cha nyuma, matatizo ya uti wa mgongo, matatizo ya tezi dume pia nayo yametajwa kuhusika na tatizo hili.

Tatizo la kiakili jamii: Hapa tunaona matatizo kama msongo wa mawazo, matatizo ya kiuhusiano (mume na mke au mtu na mpenzi wake), matatizo ya ajira, ya kifedha, ukichaa au uwendawazimu. Matatizo mengine yanasababishwa na uvutaji sigara, unywaji wa pombe, ukosefu wa usingizi wa kutosha na utumiaji holela wa dawa.

Msongo wa mawazo na hofu: Msongo wa mawazo na woga au hofu pia vimeonekana kuwa ni tatizo kubwa katika suala zima la upungufu wa nguvu za kiume au kushindwa kuwa na nguvu za kiume (hasa msongo wa mawazo unapokuwa katika suala zima la ndani ya kifamilia au suala la kifedha)

Tunaweza kusema kuwa ili kuweza kupata suluhisho la kudumu daktari au muuguzi anayekutana na mgonjwa wa namna hii ni lazima aweze kubaini tatizo na kutafuta mbinu za kiushauri nasihi ili kuweza kupata suluhisho.

Kama tatizo la upungufu wa nguvu za kiume litakuwa limeingia au kuangukia katika makundi mawili yaani mgonjwa kuwa na tatizo physical na tatizo psychological basi tatizo hili huenda likawa gumu zaidi tofauti na likiwa katika kundi moja.

Tunashauri wale wote wenye tatizo hili waende hospitali mapema kuonana na wataalam na kuwaeleze matatizo bila kuficha ili daktari aweze kuwasaidia na hivyo kupata suluhisho la kudumu la tatizo husika.

Kinga: Mwanaume anaweza kujikinga na tatizo hilo kuwa na afya nzuri, kula lishe kamilifu, kupunguza uzito kwa mwenye uzito mkubwa, kuacha kuvuta sigara, kufanya mazoezi mara kwa mara, kuacha pombe au utumiaji wa dawa za kulevya, kuacha utumiaji wa dawa kiholela (dawa za kujinunulia ovyo ovyo).

Pia kuhakikisha unapata tiba haraka kwa anayesumbuliwa magonjwa mbalimbali yakiwemo moyo na sukari.

MatibabuMatibabu kulingana na tatizo lako yapo endapo utafika hospitali mapema. Ni hatari kuamua kujinunulia dawa madukani au mitaani na kumeza kabla ya uchunguzi wa tatizo lako kwani unaweza kupata tatizo lakini halihitaji vidonge pekee.

Uchunguzi wa kina na ushauri stahiki na mahusiano mazuri kati yako na daktari wako pamoja na kufuata kanuni zote za afya ndiyo njia bora na pekee ya kuweza kupata suluhisho lako.

Kama tatizo lako ni msongo wa mawazo utokanao na ajira au mambo ya kifedha jiunge na vikundi vidogovidogo vya ujasiriamali katika kuanzisha biashara au kujiajiri ili kuweza kujikwamua katika hali ya kiuchumi.

Maoni au maswali tuma kwa simu 0713247889 au kwa baruapepe: afya@jamboleo.net

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI