Wema Sepetu Alivyorudisha Kadi ya CCM na Kujiunga Chadema


STAA wa filamu Bongo, Wema Isac Sepetu, leo Ijumaa, Februari 24, 2017 ametangaza rasmi kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kujiunga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Tukio hilo limefanyika wakati Wema alipokuwa akizungumza na wanahabari nyumbani kwa mama yake mzazi, Bi. Mariam Sepetu maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam na kurushwa moja kwa moja (LIVE) kupitia Global TV Online.
Wema amekabidhi kadi ya CCM kwa Diwani wa Ubungo na Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob huku akitangaza kujiunga na CHADEMA na kusema siku za hivi karibuni atachukua kadi zake.
Mbali na Wema, mama yake Mariam Sepetu naye amerudisha kadi ya CC ambayo alikuwa ameilipia hadi mwaka 2018 huku naye akitangaza kujiunga CCM.
“Nimeingia Chadema kwa kuwa ni chama ambacho kinapigania Demokrasia, ninachotaka kupigania katika nchi yangu ni demokrasia na siyo kingine, najua nimefanya maamuzi magumu lakini ndiyo hivyo nimeshaamua na sirusi nyuma. 
“Kuna watu wengi ambao wanapata shida huko nje kama navyopata mimi kwa sasa lakini wanashindwa kuondoka, nimeingia kwenye vita, nipo tayari ‘kupigana’. Alisema Wema.
PICHA NA KELVIN SHAYO | GLOBAL TV ONLINE

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA