Zealandia: Kuna bara la nane chini ya New Zealand?


Mount CookHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMlima Cook, mlima mrefu zaidi New Zealand - na Zealandia
Unayafahamu mabara yote saba? Jiandae sasa, kuna bara jingine ambalo huenda likaongezwa.
Bara hilo limependekezewa jina Zealandia.
Ni sehemu kubwa ya ardhi ambayo inakaribia kabisa kufunikwa na maji ya bahari kusini magharibi kwa bahari ya Pasifiki.
Kinachoonekana kwa sasa ni sehemu ya juu pekee ya milima kwenye bara hilo, ambayo hujitokeza juu ya maji ya bahari kwama visiwa ambavyo huitwa New Zealand.
Wanasayansi wanasema sehemu hiyo ya ardhi inatosha kuitwa bara na sasa wamefufua juhudi za kutaka litambuliwe rasmi kama bara.
Kwenye makala waliyochapisha katika jarida la masuala ya jiolojia Marekani la Geological Society of America, watafiki hao wanasema ukubwa wa Zealandia ni kilomita milioni tano mraba. Hiyo ni kama theluthi mbili ya bara lililo karibu la Australia.
Map of ZealandiaHaki miliki ya pichaGNS
Takriban 94% ya sehemu hiyo ya ardhi imo chini ya maji ya bahari na ni visiwa vitatu pekee vilivyochomza juu ya maji ambavyo hufahamika kama Visiwa vya Kaskazini na Visiwa vya Kusini nchini New Zealand na visiwa vya New Caledonia.
Huenda ukadhani ardhi kuwa juu ya bahari ni kigezo muhimu cha sehemu ya ardhi kuitwa bara, lakini watafiti hao wanaangazia sifa tofauti zikiwemo.
  • Mwinamo wa maeneo yanayopakana na bara hilo
  • Eneo kuwa la kipekee kijiolojia
  • Hali kwamba eneo husika linaweza kutenganishwa na maeneo mengine
  • Kuwa na gamba lake kuwa na pana kuliko gamba la kawaida baharini
New Zealand aerial viewHaki miliki ya pichaESA/NASA
Image captionPicha ya New Zealand kutoka angani ambayo ilipigwa na mwana anga Tim Peake
Mtafiti mkuu, mwanajiolojia kutoka New Zealand Nick Mortimer, amesema watafiti wamekuwa wakitafuta data ya kutetea Zealandia kutambuliwa kuwa bara kwa miongo miwili.
Iwapo mpango wao utafanikiwa, wachapishaji wa vitabu wanafaa kuwa na wasiwasi kwamba watahitaji kufanya marekebisho?
Kumbuka miaka michache iliyopita Pluto iliondolewa kwenye orodha ya sayari kwenye mfumo wa jua.
Hakuna kundi lolote la kisayansi lenye wajibu wa kutambua mabara.
Hivyo, itachukua muda kwa bara hilo kutambuliwa rasmi na kukubalika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.