BASATA YAUFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO…


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo ‘WAPO’ uliombwa na msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kutumika kwa namna yoyote ile.
Kwa mujibu wa BASATA, kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kusimami kazi za Sanaa na mamlaka za kishirika kuhakikisha yote yafanyikayo katika tasnia ya Sanaa hayaachi taifa na wasanii katika hali zisizokuwa salama.
Katika kutekeleza majukumu haya, Baraza linahakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi zozote za sanaa.
Kwa muda huu, BASATA linawakumbusha wasanii na wadau wote wa kazi za sanaa kuzingatia ubunifu wa hali ya juu kufanya kazi za Sanaa, hata kufikisha jumbe mbalimbali za kufundisha, kuelemisha, kuburudisha na kuonya.
Baraza linawaonya wale wote wanatumia kazi zilizopigwa marufuku. Ikumbukwe kuwa kutumia kazi zilizopigwa marufuku ni ukiukwaji wa sheria za nchi ambapo hatua kali zitachukuliwa juu yao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU