Canada kuhalalisha bangi ifikapo mwaka ujao


Canada kuhalalisha bangi ifikapo mwaka ujaoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionCanada kuhalalisha bangi ifikapo mwaka ujao
Matumizi ya bengi kwa kujiburudisha yatahalalishwa nchini Canada ifikapo tarehe mosi Julai mwaka 2018.
Serikali ya Canada itawasilisha mswada wa kuhalalisha bangi ifikapo Aprili kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la CBC.
Taarifa ziliiambia CBC kuwa wanachama wa chama tawala cha Liberal hivi majuzi walijulishwa kuhusu mswada huo.
CBC imesema kuwa sheria hizo mpya zitaambatana na mapendekezo yaliyotolewa na jopo lililoteuliwa na serikali.
Baadhi ya mapendekezo hayo ni kuwa Canada itaruhusu kuuzwa kwa bangi wa kujiburudisha kwa watu walio na zaidi ya umri wa zaidi ya miaka 18,.
Canada kuhalalisha bangi ifikapo mwaka ujaoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionCanada kuhalalisha bangi ifikapo mwaka ujao
Jopo kazi hilo pia lilipendekeza kuwa watu wazima wataruhusiwa kupanda hadi mimea minne ya bangi na wamiliki hadi gramu 30 ya bangi iliyokaushwa.
Kwa mujibu wa CBS, serikali itasimamia kusambazwa wa bangi na kuwapa leseni wazalishaji.
Ahadi wa waziri mkuu Justin Trudeau, ya kuhalalisha bangi imechochea uvumi katika sekta hiyo.
Wazalishaji kama makampuni ya Aphria, OrganiGram Holdings, na Canopy Growth, ambao ni wazalishaji wakubwa zaidi wa bangi ya kutibu, yamekuwa vipnzi kwa wawekezaji wa hisa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*