KOMPYUTA YENYE SIRI YA KIKOSI CHA KUMLINDA RAIS WA MAREKANI YAIBWA


Kompyuta ya kikosi cha kumlinda rais wa Marekani inayoripotiwa kuwa na michoro ya jumba la Trump Tower, na taarifa zingine za siri imeibwa kutoka kwa gari la afisa mmoja mjini New York.
Hata hivyo kikosi hicho cha kumlinda rais kinasema kuwa kompyuta hiyo huikuwa na taarifa za siri.
Lakini wanasema kuwa ina taarifa kuhusu uchunguzi wa aliyekuwa mgomea wa Democratic Hillary Clinton kutumia barua pepe ya kibinafsi.
Kwa sasa polisi wanachunguza kamera za siri kuweza kumtambua mshukiwa.
Shirika la ABC lilisema kwa gari la ajenti lililengwa katika eneo la Bath Beach kwenye mtaa wa Brooklyn.
CBS nayo ilisema kuwa kampyuta hiyo ilikuwa na taarifa muhimu kumhusu Papa Francis
Taarifa za polisi zililiambia gazeti la The York Daily News, kuwa taarifa zilizo kwenye kompyuta hiyo ni za siri kubwa.
Kompyuta hiyo inaripotiwa kuibwa kutoka kwa mkoba uliokuwa ndani ya gari. Mkoba huo hata hivyo umepatikana lakini kompyuta yenyewe bado inatafutwa.BBC
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI

KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI