Ndege yenye kasi zaidi duniani kutengenezwa, Australia hadi Marekani zitatumika saa sita

March 28, 2017 millardayo.com inakusogezea story inayoihusu Kampuni ya Boom Supersonic’s XB-1 ambayo imeanza kutengeneza ndege ya kwanza yenye kasi zaidi duniani ambayo itaweza kumsafirisha mtu kutoka Bara la Australia mpaka America ya Kaskazini kwa muda wa saa sita tu.
Utengenezaji wa ndege hiyo utagharimu zaidi ya Dola million 329 za Marekani na inatarajia kukamilika mwaka 2020 ambapo CEO wa kampuni hiyo Blake Scholl aliiambia Daily mail kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kuruka umbali wa zaidi ya futi 60,000 kutoka usawa wa Bahari ambao ni umbali mrefu sana ukilinganisha na ndege za kawaida.
Ndege hiyo itakuwa na kasi zaidi ya Concord ambayo inajulikana kama ndege yenye kasi zaidi duniani na itakua na seat 45 na safari zake zitagharimu Dola 6,600 za Marekani na itaweza kumsafirisha mtu kutoka Japan mpaka San Francisco kwa muda wa saa tano tu wakati ndege ya kawaida husafiri kwa zaidi ya saa 10 na dakika 48.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI