RAIS MAGUFULI AMKINGIA KIFUA MAKONDA

Matukio yote hayo ya mapema na sauti iliyopazwa jana, ilitegemewa leo mkuu wa mkoa wa Dar aidha aachie ngazi kwa hiari au kwa kushurutishwa. Tofauti na matarajio, Rais Magufuli ametaka mkuu wa mkoa achape kazi na amewaasa wana Dar kuacha kutekwa sana na udaku japo ni uhuru wao lakini wajikite katika ujenzi wa uchumi.

Rais amesisitiza watu wanahangaika kuposti mitandaoni na wapo waliodiriki kumpangania lakini yeye ni Rais anayejiamini na ndie anapanga nani akae wapi.

Leo kulikuwa na matukio mawili makubwa, likitanguliwa na mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media, Ruge Mutahaba kukiri uvamizi uliofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda kwa kutumia vyombo vya dola na kulaani Kitendo hicho akifuatiwa na waziri wa habari, Nape Nnauye ambae naye alisema kitendo hicho kimenajisi tasnia ya habari mwisho mwenyekiti wa MOAT, Reginald Mengi kupigilia msumari kwa kuwataka waandishi wasirudi nyuma na wasiogope.

Rais Magufuli amesema kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiyo mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini.

Mkuu huyo wa nchi amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo badala ya kupoteza muda kufuatilia udaku kwenye mitandao.

"Watu wa Dar es Salaam tumejielekeza sana kwenye udaku ambao hausaidii maendeleo. Udaku ambao haumalizi hata foleni ya Dar. 

"Ningefurahi sana huko kwenye mitandao kama tungekuwa tunajadili jinsi ya kufanya mambo ya maendeleo.


"Mimi sionyeshwi njia ya kupita na mtu. Njia ya kupita tayari nilishaonyeshwa na ilani ya chama changu.


"Kuandikwa kwenye mitandao hata mimi ninaandikwa, kwa hiyo nijiuzulu? Kuandikwa kwangu mimi siyo tija bali kuchapa kazi.


"Kuna wengine mmefikia hata hatua ya kunipangia. Nasema mimi ukinipangia ndio umeharibu
"Vitu ambavyo havina msingi vinachukua muda wetu mwingi sana. Mara upost hiki, mara uweke kile.


"Watanzania mjue kampeni zimeshakwisha. Ulie, ugaregare lakini Rais ni mimi John Pombe Magufuli na kwangu ni kazi tu
"Mimi ni rais ninayejiamini, sipangiwi mambo ya kufanya. Hata fomu ya kugombea nilikwenda kuichukua peke yangu, kwa hiyo Makonda wewe chapa kazi,"
 amesema Rais Magufuli.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR