WABUNGE Dk. KAFUMU, VICK KAMATA WAJIUZULU

Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya viwanda na biashara Mhe.Dr.Dalaly Peter Kafumu (CCM) ametoa rai ya kujiuzulu uongozi wa kamati hiyo, kufuatia kuandamwa na baadhi ya viongozi wa serikali kufuatia nia yake ya kumtembelea Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema alipokuwa gerezani.

Dr.Kafumu ametoa rai hiyo kwenye kikao cha kwanza cha kamati ya viwanda na biashara kilichoanza leo. Kafumu na Makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Vicky Kamata walipanga kumtembelea Mhe.Godbless Lema gerezani kwa kuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.

IMG_4326.JPG 

Baada ya taarifa hiyo, viongozi mbalimbali walisikika kukosoa utaratibu huo na kuwaita wasaliti. Kafumu amesema haoni sababu ya wao kuitwa wasaliti kwa kuonesha nia ya kumtembelea mjumbe mwenzao wa kamati. "Mhe.Lema ni mjumbe mwenzetu wa kamati hii, kwanini ionekane ni dhambi kumtembelea alipopata matatizo?" Dr.Kafumu amewahoji wajumbe wa kamati hiyo?

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Vicky Kamata amesema kuwa ikiwa Dr.Kafumu atajiuzulu uenyekiti, naye atajiuzulu nafasi yake ya makamu mwenyekiti.

IMG_4325.JPG 

SOURCE: Nimezungumza na wajumbe wa Kamati, wamedhibitisha taarifa hizo.!
=======

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*