KONGAMANO LA MOTHER & CHILD GALA 2017 LAFANA DAR

 Watoto wakifurahia wakati wa Kongamano la Mama na Mtoto (Mother & Child Gala 2017) lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa  Danken House, Mikochezi Dar es Salaam. Kongamano hilo liliandaliwa na Kampuni ya 247 Communications kwa uratibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Dorothy Kipeja na Organising Partiner, Sarah Mauki. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Na Richard Mwaikenda

MTALAAM wa Ushauri wa Mahusiano na Saikolojia, Dk. Chris Mauki amesema migogoro ya wazazi husababisha watoto kufeli mitihani shuleni.

Kauli hiyo aliitoa wakati akitoa mada katika kongamano la Mama na Mtoto (Mother & Child Gala 2017) la kuwapa uwezo akina mama kuwalea watoto kimaadili ili wawe wazazi wazuri wa baadaye.

Akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Danken House, Mikocheni, Dar es Salaam, alisema watoto wanaoshuhudia mara kwa mara ugomvi wa wazazi wao huathirika kiakili kitendo ambacho husababisha wafanye vibaya  masomo darasani.

Aliwaasa wazazi kuacha tabia hiyo kwani inaharibu maisha ya baadaye ya watoto ambao kwa asilimia kubwa huathirika kisaikolojia na kusababisha kutokuwa makini kwenye masomo.

Alisema jambo lingine linalowaathiri watoto ni migogoro ya wazazi inayosababisha ndoa kuparanganyika kwa kila mmoja kuishi kivyake, hivyo kuwafanya hata watoto kulelewa na upande mmoja wa wazazi.

"Watoto wanahitaji kupumzika moyoni, kupendwa moyoni, hivyo mnatakiwa kuwasikiliza watoto siyo kuwasikia, sikilizeni matatizo yao na kuyatatua kwa pamoja, huo ndiyo ni msingi mzuri wa maisha yao ya baadaye."Alisema Dk. Mauki.

Katika kongamano hilo lililoandaliwa na Kampuni ya 247 Communications, akina mama na watoto walipata nasaha zingine kutoka kwa Sadaka Gandi na mhamasishaji Lillian Mwasha pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vinjari, Andrew Mboma ambaye aliwasihi wazazi kuwaelimisha watoto kuhusu umuhimu wa kujua vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kupata wasaa wa kuvitembelea, pia kuipenda nchi yao.

Wazazi na watoto walijumuika pamoja kucheza muziki kwa kuongozwa na msanii Msami  Jovan 'Msami' tukio ambalo lilifurahiwa na kila mtu ukumbini hapo.Kongamano hilo liliratibiwa na Dorothy Kipeja na Sarah Mauki.



 MC wa Kongamano hilo, Llian Mwasha akitoa maelekezo kwa watoto wakati wa kongamano hilo
 Watoto wakicheza kwa furaha wakati wa kongamano hilo
 Wazazi na watoto wakicheza muziki
 Mtoto Mischa Ngoshani akisoma kwa makini hotuba kwa ajili ya watoto wenzie na wazazi 
 Akina mama wakiwa na furaha
 Mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Mother & Child Gala,  Dorothy Kipeja (kushoto) akiwa na Organising Partiner wa Mother & Child Gala, Sarah Mauki pamoja na watoto wao
 Washiriki wa kongamano hilo wakipata breakfast

 MC Lillian akiwapa maelekezo watoto waliofungwa vitambaa kabla ya kwenda kuwatambua mama zao
 Watoto wakiwa na mama zao baada ya kuwatambua ambapo wengine waliwatambua kwa kuwanusa na wengine kwa kuwagusa
 Wazazi na watoto wakicheza kwa furaha
 MamaManka Alphonce akitoa uzoefu wake wa kulelea watoto kimaadili
 Mwezeshaji  Sadaka Gandi akieleza umuhimu wa wazazi kuwalea watoto kimaadili ili waweze kuwa wazazi wema katika Kongamano la Mama na Mtoto (Mother & Child Gala) kwenye Ukumbi wa Danken Mikocheni Dar es Salaam juzi. Kongamano hilo liliandaliwa na Kampuni ya 247 Communications
 Msanii Msami Jovan 'Msami' akiwafundisha watoto kucheza muziki wakati wa Kongamano la jinsi wazazi wanavyotakiwa kuwalea watoto kimaadili kwa kuzungumza nao kwenye Ukumbi wa Danken House Mikocheni Dar es Salaam juzi. Kongamano hilo la Mama na Mtoto (Mother & Child Gala) liliandaliwa na Kampuni ya 247 Communications. 
 Watoto wakiwa na zawadi zao walizogawiwa na Benki ya NMB
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vinjari, Andrew Mboma  akimpongeza Betha na mwanawe Latifa Zahor walioshinda bahati nasibu ya kwenda kuvinjari Zanzibar kwa siku mbili kwa gharama ya kampuni hiyo. Katikati ni Dorothy Kipeja.
 Ofisa Mafunzo  Idara ya Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS, Waziri Ramadhan akielezea umuhimu wa wazazi na watoto kujiunga na kampuni hiyo.
 Msanii Msami Jovan 'Msami' akiwafundisha watoto kucheza muziki wakati wa Kongamano la jinsi wazazi wanavyotakiwa kuwalea watoto kimaadili kwa kuzungumza nao kwenye Ukumbi wa Danken House Mikocheni Dar es Salaam juzi. Kongamano hilo la Mama na Mtoto (Mother & Child Gala) liliandaliwa na Kampuni ya 247 Communications. 
 Msanii Msami Jovan 'Msami' akiwafundisha watoto kucheza muziki wakati wa Kongamano hilo.
 Mtaalamu wa Ushauri wa Mahusiano, Dk. Chris Mauki akitoa mada katika kongamano la Mama na Mtoto (Mother & Child Gala), Dar es Salaam juzi, kuhusu migogoro ya wazazi inavyosababisha watoto kufeli mitihani shuleni.  Kongamano hilo liliandaliwa na Kampuni ya 247 Communications
Organising Partiner wa Mother & Child Gala, Sarah Mauki akiwashukuru akina mama na watoto kwa kushiriki kongamano hilo na hatimaye kuhitimisha.
 Mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Mother & Child Gala,  Dorothy Kipeja (kushoto) na Organising Partiner wa Mother & Child Gala, Sarah Mauki wakiwazawadia baadhi ya akina mama 
Akina mama na watoto wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kongamano kumalizika;

Kwa mawasiliano zaidi piga kwa Mmiliki wa Blog hii Richard Mwaikenda namba 0715264202/0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA