Na Mwandishi Wetu
MBUNGE
wa Jimbo la Mchinga, mkoa wa Lindi, Hamidu Bobali ametoa vifaa vya michezo kwa
timu za Aston Villa ya kata Mchinga Two na Timu ya Waasi FC ya kata ya Milola
pamoja na mipira minne ikiwa ni ahadi yake kwa timu hizo.
Bobali
alitekeleza ahadi hiyo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi aliyoifanya hivi
karibuni kwenye jimbo hilo ambapo alipokea kero na changamoto mbalimbali kutoka
kwa wananchi.
Akizungumza
baada ya kutoa vifaa hivyo vya michezo Bobali alisema matarajio yake ni kuona
soka la Mchinga na Lindi kwa ujumla linakuwa hivyo atahakikisha timu zote
zinapata vifaa hivyo.
“Mimi
ni mchezaji wa mpira hivyo naamini katika michezo ndio maana nimeamua
kutekeleza ahadi yangu ya kuwanunulia vifaa ambavyo waliniomba naamini
hawataniangusha,” alisema.
Mbunge
huyo alisema ni jukumu la Serikali kuweka mazingira ya viwanja vizuri ili
kuhakikisha kuwa vijana hao wanashiriki kwani michezo ni moja ya ajira.
Alisema
ataendelea kusaidia timu mbalimbali ambapo kwa sasa ni mmoja wa wafadhili wa
ligi ya Kanda ya Kusini ambayo inashirikisha timu za kanda hiyo.
Comments