Newcastle yarejea ligi kuu ya England


NewcastleHaki miliki ya pichaPA
Image captionAyoze Perez mfungaji wa mabao mawili ya Newcastle
Klabu ya Newcastle United msimu ujao watakipiga katika ligi kuu ya England ya baada ya kupanda tena daraja kutoka Championship kwa kuichapa timu ya Preston kwa mabao 4-1.
Mshambuliaji wa Newcaste Ayoze Perez ndie aliyeanza kuiandika timu yake goli la kuongoza katika dakika ya saba ya mchezo,Katika dakika ya kumi na nne Preston wakachomo goli hilo kupitia kwa mshambuliaji wake Jordan Hugill,
Kiungo Christian Atsu akaiongezea Newcastle bao la pili katika dakika ya arobaini na tano ya kipindi cha kwanza, katika dakika ya sitini na tano winga Matt Ritchie akaongeza bao la tatu kwa vijana wa Rafa Benitez kwa mkwaju wa penati.
NewcastleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWachezaji wa Newcastle wakishangilia ushindi
Mshambuliaji Ayoze Perez tena akashindilia msumari wa mwisho uliowahakishia Newcastle kurejea tena katika ligi kuu msimu ujao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA