BALOZI SEIF ALI IDDI AONGOZA WADAU HABARI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI ZANZIBAR


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wadau wa Habari kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani hapo katika Chuo cha Habari Kilimani Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga, kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Mitawi.
 Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar Omar akitoa ufafanuzi juu ya Umuhimu wa Wanahabri kuzingatia suala la Amani katika uandishi wao wa kila siku.
 Viongozi wa Meza Kuu kutoka kulia Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga, Mkuu wa Mkoa Mjini Maghribi Mh. Ayoub, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif, Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Nd. Hassan Mitawi wakifuatilia hafla ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari hapo Kilimani.
 Kikundi cha Utamaduni cha Mkoa Mjini Magharibi kilitoa Burdani katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari hapo katika Ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Mjini Zanzibar.
 Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga akitoa salamu kwenye hafla ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani Mjini Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Abdulla Hassan Mitawi akifafanua jambo kwenye maadhmisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Dunani.
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud  akijiandaa kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari yaliyofanyika katika Viunga vya Chuo cha Habari Zanzibar kiliopo Kilimani Mjini Zanzibar.
 Washiriki mbali mbali waliohudhuria  Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani yaliyofanyika katika chuo cha Habari Zanzibar  kilipo Mtaa wa Kilimani.
Balozi Seif Ali Iddi kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Habari Nchini mara baada ya kufungua mdahalo wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga, kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Mitawi. Picha na – OMPR – ZNZ.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU