Bintiye Mugabe ateuliwa katika bodi ya udhibiti vyombo vya habari



Bona Mugabe-ChikoreHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBi Chikore alihitimu katika chuo kikuu Singapore
Binti wa kipekee wa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Bona Mugabe-Chikore, ameteuliwa katika bodi ya udhibiti vyombo vya habari na sekta ya filamu nchini katika kile ambacho wakosoaji wanasema ni hatua ya kusaka taarifa zinazoipinga familia hiyo, hususan katika mitandao ya kijamii.
Msemaji wa polisi Charity Charamba pia atahudumu katika bodi hiyo ya watu 11 iliyoteuliwa na waziri wa mambo ya ndani Ignatious Chombo, pamoja na wawakilishi wa makundi ya makanisa, wataalamu wa sheria na uhasibu na vioongozi wa kitamaduni, anaarifu mwandishiw a BBC kutoka mji mkuu, Harare.
Shirika la kitaifa la habari imesema bodi hiyo itadhibiti na kukagua vyombo vya habari na sekta ya filamu nchini na kulenga "matumivi mabaya ya mitandao ya kijamii wakati pia ikizingatia uchaguzi mkuu unaowadia mwaka ujao".
Bi Mugabe-Chikore amesomea Singapore, na ana shahada ya uzamili katika masuala ya usimamizi, hususan wa mabenki na fedha.

Mada zinazohusiana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI