4x4

HABARI MPASUKOOOOO. AJALI YA DALADALA NA LORI YASABABISHA VIFO NA MAJERUHI DAR

AJALI ya daladala na Lori imetokea leo asubuhi jijini Dar es Salaam na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Ajali hiyo iliyohusi daladala linalofanya safari za Msasani- Mbagala limegongana na lori la Azania eneo la Mtava, Barabara ya Nyerere.

Kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba daladala lililokuwa linatokea Gongo la Mboto kwenda Msasani liliharibika vibaya upande wa mbele baada ya kuligonga lori lililokuwa linakatiza barabara kutokea upande wa kushoto kuingia kwenda Tazara..

Miili ya waliokufa na majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa Hospitali ya Muhimbili.

Habari zaidi tutaendelea kuwaletea kwa kadri tutakavyokuwa tunazipata
Post a Comment