Her Initiative yawakutanisha pamoja wasichana katika Tamasha la ujasiriamali, uvumbuzi na ajira (PANDA)

Her Initiative iliyojulikana hapo awali kama Teen Girls Supportive Initiative (TGSI) iliandaa mkutano ujulikanao kama Panda, uliowakutanisha pamoja wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na wanahabari, lengo likiwa ni kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo.

Her Initiative ni asasi ya wasichana ambapo wao wenyewe ndio mhimili wa maongezi, ambayo inawapa wasichana nafasi ya kuwakilisha na kusimamia maswala yao wenyewe ya kiuchumi, kielimu, kiutamaduni na kiafya. Zaidi inamjengea uwezo msichana kwa kutafuta suluhu ya changamoto zake mwenyewe bila kutegemea watu wengine. Vyote hivi hufanyika kupitia kampeni, matamasha, semina na kuwapa msaada wa mahitaji ya kielimu, kiuchumi na kiafya kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali.
Faraja Nyalandu mmiliki wa Shule Direct ambaye ndie alikuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano huo akiwsihi wanafunzi kuwa na nidhamu ya pesa kwa kutumia kidogo na kuwekeza zaidi. 

Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Her Initiative, Maureen Richard aliwataka Wasichana kujishughulisha na vitu mbali mbali, kwani Uwezo wanao na Panda ni mwanzo wa maendeleo mengi zaidi kwa wasichana. "Nina wasihi wasichana wajitambue, wajithamini na wachakarike pia watumie fursa walizonazo kujikwamua kiuchumi" alisema Maureen Richard.

Mkutano huo ulifanyika mapema wiki iliyopita katika ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam. Watu mbalimbali mashuhuri walikuwepo kuwapatia motisha na ushauri wasichana hao, wakiongozwa na Faraja Nyalandu mmiliki wa Shule direct (mgeni rasmi), Elizabeth Muro  "mshauri mkuu wa Commercial Bank of Africa ", Jokate Mwegelo mmiliki wa "Kidoti", Martin Kadinda "mshindi wa ubunifu wa mavazi" , Philip Makoye "mmiliki wa Mak Juice".
Mwanzilishi wa Her Initiative ambaye kwa sasa ni Kiongozi wa Nguvu ya Binti na Mtangazaji wa vipindi vya Fema, Lydia Charles akitoa neno kwa wasichana wenzake.

Mkutano huo wa PANDA 2017 ulidhaminiwa na  TECNO MOBILE , EFM , RACHEL'S CHOICE Pamoja na MICHUZI MEDIA GROUP.
Philbert makoye (Makjuice) akiwasihi wasichana kutumia nafasi wanazozipata vizuri na kutokukata tamaa ya malengo walioyapanga .
Jokate Mwegelo alimpongeza Lydia kwa ujasiri na Moyo wa kufanya kazi ingawa alipitia changamoto nyingi. Pia alitoa wito kwa wasichana kuiga mfano kutoka kwa muanzilishi wa taasisi hiyo, Lydia Charles ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa vipindi vya Fema.
Mwenyekiti mpya wa Her Initiative Moureen Richard (Kati) akiwa pamoja na mzungumzaji Elizabeth Muro (kulia) na Lydia Charles (kushoto).
Kwenye tamasha hilo la Mwaka 2017 pia walitambua wasichana wanaojituma katika Nyanja tofauti tofauti ambao ni Nandy, Diana Mbogo, Tuli Mwampanga, Jihan Dimack, Genevieve Mpangala, Amina Sanga , Shamira Mshangama mwanafunzi kutoka chuo cha Dar es salaam mwandishi wa vitabu.
Martin Kadinda akiongea na wasichana juu ya kuwa tofauti katika maisha na kutumia kipaji ili kujikwamua kiuchumi .
Baadhi ya wasichana walioshiriki katika tamasha hilo.
Timu ya maaadalizi ya tamasha hili kutoka shirika la Her Initiative.
wasichana wa walioshiriki katika tamasha hilo wakifurahia.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*