HOSPITALI YA AGA KHAN YANZISHA USHIRIKIANO NA ALY KHANI YA INDIA

Abraham Ntambara
HOSPITALI ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam wameanzisha ushirikiano na Hospitali ya Aly Khani ya Mjini Mumbai India kwa lengo la kuboresha huduma za afya nchini Tanzania hususani kwenye upasuaji wa mifupa katika nyonga na magoti.

Hayo yalibainishwa jana jinini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Aga Khan, Sisawo Konteh wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema ushirikiano huo utakuwa wa muda mrefu.

“Ndugu zetu hawa kutoka Mumbai India tumekubaliana waje hapa kuangalia namna tunavyotoa huduma mbalimbali, ili tuone wapi tunaweza kuboresha hususani huduma zinazoweza kufanywa nchini zifanyike,” alisema Konteh.

Aliongeza kuwa kutokana na ushirikiano huo utawapa fursa madaktari nchini kuweza kuongeza ujuzi katika upasuaji kutoka kwa madaktari bingwa wa hosspitali wa Aly Khan kwani uhusiano huo utakuwa wa muda mrefu.

Muuguzi Mkuu wa Aga Khan Lucy Hwai alibainisha kuwa wageni hao wamekuja ili kuboresha uhusiano uliopo baina yo hospitali hizo.

Alieleza kuwa kwa sasa kuna mladi wa ujenzi unaendelea wa jingo linalogharimu sh. bilioni 1.7 ambapo alifafanua kuwa litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua vitanda 170.

Alisema kutokana na idadi hiyo watahitaji kuwa na wataalamu wakuweza wengi ambao wataweza kufanya huduma  za matibabu kwa wa gonjwa watakao kuwa wakiripoti hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.

“Linatarajia kukamiliaka mwakani kuanzia mwezi wa sita, ndipo ushirikaono utakapotakiwa zaidi na hii itasaidia sana wagonjwa ambao walitakiwa kupelekwa India wataweza kupatiwa matibabu nchini,” alisema Hwai.

Hwai alisisitiza kuwa ili kuhakikisha usharikano huo unaboresha huduma za afya, utaenda sambamba katika kutoa na kuimarisha elimu kwa madaktari nchini ili watanzania wapate faida katika huduma za afya.

Aidha alisema kuanzia jana na leo watatoa huduma ya upasuaji wa nyonga na magoti kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka India ambapo alieleza kuwa madaktari hao watakaa watakuwepo hadi Mei 8 mwaka huu.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa hospitali ya  Prince Aly Khan Sanjay Oak, alisema wameanzisha ushirikiano huo ili kusaidiana kwa pamoja katika kutoa huduma za upasuaji nchini.

Alisema kwa kipindi sasa hatua katika huduma za upasuaji zimekuwa zikibadilika kutokana na maendeleo ya teknolojia ambapo aleleza kuwa yeye amekuwa akifanya huma hiyo kwa zaida ya miaka 30 na ameshafanya upasuaji kwa watoto zaidi ya 3000.

MWISHO
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)