HOTUBA FUPI YA,RAIS MAGUFULI BAADA YA KUPOKEA RIPOTI YA TUME YA UCHUNGUZI WA MCHANGA WA MADINI PAMOJA NA HATUA ALIZOZICHUKUA


..Endelea....Tulitumia vifaa vyote katika ulinzi lakini wapo waliojitokeza kutaka kuingilia uchunguzi huu na bahati nzuri majina yote tunayo, wapo wengine mnawajua wenyewe wakibwatuka wengine kwenye mitandao, wamepewa fedha.
Ndugu zangu tuko kwenye vita na vita ya uchumi ni mbaya sana, mabilioni ya fedha haya ambayo nchi yetu imepoteza, dhahabu tani tani 7.8 hadi 13.16 kwa kontena 277. Tani 15.5 ni malori mawili na land rover moja. Malori mawili ya tani 7 yanaleta tani 14, labda na pick up zote umezipaki pale na hio ni kwa makontena 277.
Kuna tume inayotaka kujua ni makontenayanasafirishwa mangapi, haraka haraka ni makontena 250 na 300 kwa mwezi, kwa mwaka zaidi ya makontena 3600.
Ni kitu cha kuumiza mno na kwa hili watanzania wote tushikamane, hospitali watu wanakosa madawa, mashuka, shule watu wanakosa madawati, hela za treni mpaka tukope kumbe kuna hela zinamwagika hapa.
Nilimfukuza katibu mkuu wa nishati na madini alipoulizwa na kamati ya wabunge kiasi cha dhahabu kilichopo, ni aibu kwa mtu aliesomeshwa na watanzania.
Bilioni 676 hadi trilioni 1.5 tunzazipoteza watanzania, madini mengine hawakujali hata kuyarekodi(Nipe ile document). Tunaweza tukaona kwa miaka kwa 17, tulipaswa kuwa donor country kwa vitu tulivyopewa na Mungu.
Hauwezi ukashangaa katika wizara hizi ndio nilichagua watu waziri wa kuziendesha, kuna tume iliundwa miaka ya nyuma, walidanganya kuna smelter ziko nchi fulani, walipoenda wakaishia hotelini. Smelter sio tatizo kwenye ripoti, inaonyesha kampuni nyingi zinazoweza kuuza smelter, viongozi hawakuchukua juhudi za kununua smelter.
Sera ya taifa ya madini ya mwaka 2009 inasema haja ya kununua smelter, viongozi wa hizo wizara hawakufanya juhudi, kwanini TMAA wapime kidogo halafu wanakuja kuweka tu seal wakati hujui kilichowekwa ndani, kwanini?
Kwanini wasimamizi wasimamizi wa TMAA ambao ni wizara hawakushtukia? Kwanini bodi ya TMAA haiwakushtukia? Inawezekana nikajiuliza maswali mengi majibu yasipatikane. Inawezekana yakaletwa na tume nyingine, nilienda na wenzangu kuteta kidogo, Haiwezi kupita hivi hivi.
Ripoti hii ikipita hivi hivi tutakuwa watu wa ajabu sana, tutafanya kitu, tunasubiri ile ripoti nyingoine.
Mapendekezo yote ya tume nimeyakubali
Bodi ya TMAA nimeivunja Rasmi
Namsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa TMAA na wafanyakazi waanze kuchunguzwa na vyombo vya dola
Shughuli zote zinazohusu madini, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vianze kutumika sawasawa.
Wizara wameshindwa kusimamia TMAA, ujenzi wa Smelter pia imeshindwa kuweka utaratibu wa kufatili haya makenikia, mbona huwa wanaenda Ulaya? Kamishna madini anafanya nini? Waziri anafanya nini?
Vyombo viwachunguze watendaji wa wizara ya madini wanaoshughulia
Nampenda sana Prof Mhongo na ni rafiki yangu, kwa hili ajitathmini na nilitaka aachie madaraka.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PADRI AUGUSTINO RAMADHANI AONGOZA IBADA YA KUMBUKUMBU YA MKE WA PROFESA SHABA DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI