IGP SIRO AOMBA SAPOTI YA WANANCHI KUKOMESHA MAUAJO KIBITI

Mwandishi Wetu
MUDA mfupi baada ya kuapishwa Ikulu Dar es Salaa, Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya, IGP Simon Sirro amesema uhalifu hauwezi kupungua kwa kulitegemea jeshi hilo pekee, bali nguvu ya pamoja inahitajika akitoa mwito kwa wananchi kushirikiana na jeshi lake.
Amesema wananchi wakitoa taarifa za wahalifu waliopo maeneo yao jambo hilo litaweza kupunguza au kuondoa uhalifu nchini.
Aidha, IGP Sirro ametaja kipaumbele chake cha kwanza kuwa ni kupambana na uhalifu na kudhibiti nidhamu kwa askari akieleza bila hivyo itakuwa vigumu kumaliza uhalifu, huku akiwaahidi kulala usingizi wa amani wananchi wa Mkoa wa Pwani kwa kufanyia kazi matukio ya uhalifu yaliyojitokeza.
Alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuapishwa na Rais John Magufuli kuliongoza Jeshi la Polisi la Tanzania.
“Uhalifu hauwezi kupungua kwa kutegemea Jeshi la Polisi pekee, tunahitaji nguvu ya pamoja ili kushinda vita hiyo, ushirikiano wa wananchi unahitajika kwa kiasi kikubwa,” alisema IGP Sirro.
Akiwa IGP wa kumi kuongoza jeshi hilo, Sirro alisema kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kulinda na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao na kwamba ni wajibu wa jeshi lake kuhakikisha Taifa lina ulinzi wa kutosha utakaowezesha wananchi kuishi kwa amani na utulivu wakifanya kazi zao bila kubugudhiwa.
“Kipaumbele cha kwanza katika utendaji wangu ni kupambana na uhalifu pamoja nidhamu ya watendaji kazi kwani bila nidhamu, kazi ya kupambana na wahalifu haiwezi kufanikiwa,”alisema IGP Sirro.
Akizungumzia matukio ya uhalifu ya mara kwa mara yaliyoambatana na mauaji mkoani Pwani, IGP Sirro alisema atafanyia kazi changamoto zinazowakabili na kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwa amani na utulivu.
IGP Sirro ambaye kabla ya uteuzi huo, alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, alimshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kushika nafasi hiyo akiahidi kufanya kazi kwa bidii na uadilifu.
Kabla ya uteuzi huo, Sirro aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, kisha Kamanda wa Kikosi cha Operesheni Maalum.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.