IGP Sirro atangaza 'vita' na wahalifu wa Mkoani Pwani

IGP mpya wa jeshi la polisi amewaita waandishi na kwanza ameomba ushirikiano wa waandishi wa habari uendelee kama walivyompa aliepita.

Amesema anawahakikishia swala la Ikwiriri na Rufiji ni la muda mfupi na yeye na timu yake ndani ya Jeshi la polisi ni lazima watapata majibu, amesema kikundi cha watu wachache hakiwezi kuwafanyia watanzania ubaya.

Amesema wanapeleka salam kuwa ubaya wanaoufanya waujibu kwa ubaya kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu wanaotumia bodaboda kufanya uhalifu, amesema hakuna mtu alie juu ya sheria. Amesema bodaboda wanapita kwenye taa nyekundu, wanapita wakiwa kwenye mshikaki. Amewapa salam kuwa ni wakati wa utii wa sheria.

Amesema watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya waache.

Watu wenye hasira kali nao wameguswa akitolea mfano wezi wa kuku na kuhoji kama kuku ana thamani sawa na mhusika. Amesisitiza kama amekosa akamatwe na apelekwe mahakamani na kusema anayejifanya ana hasira kali itamfanya aiache familia yake.

Kuhusu askari kujihusisha na rushwa, amesema hakuna askari atakaejihusisha na Rushwa na akabaki salama na kusema ameshatoa maelekezo kwa jeshi polisi kuwa atakaefanikisha kupatikana kwa wala rushwa atapata zawadi.

Ameahidi milioni kumi kwa atakaetoa taarifa sahihi kwa watu wa Kibiti, mwisho amewatakia mfungo mwema walio kwenye swaum.

Kipindi cha Mwaswali

Sirro: Polisi ni wale wale, kazi tu ifanyike ili wananchi wajue wako salama. Mimi siji na safu nyingine, ntatoka nayo wapi? Ndugu yangu mambo ya mitandao achana nayo, watendaji ni hawa hawa.

Swali: Uchache wa askari kulingana na ratio ya watanzania, una mpango wa kuongeza askari kuleta uwiano mzuri?

Sirro: Kikubwa ni swala la bajeti lakini ningependa tuongezeke, inategemea na keki iliyopo.

Swali: Mauaji ya askari mara kwa mara, mauaji haya yana nini nyuma yake?

Sirro: Haya mauaji ni ajali kazini, sio kwamba tunakufa sisi tu, hata wao wanakufa. Sisi tumeapa ndio maana najisikia vibaya sana mtu anapokamatwa na ku-resist. Ni ajali kazini na sisi huwa inatupa nguvu sana, huwa tunajipanga.

Majibu ni kuhakikisha wanamkuranga wanaishi kwa amani, vitendo vinazungumza zaidi kuliko maneno, wanaIkwiriri wasubiri majibu na itapatiakana kupitia ushirikiano. Nimeona kwenye mitandao wanalalamika nguvu kubwa imetumika, tutaangalia jinsi ya kufanya kwa sababu tusipoaminiana kazi itakuwa ni ngumu, sio muda mrefu tutapita kuzungumza na wananchi na tunajua kuna vibaraka watakuwepo. Kwa leo habari ya Ikwiriri sitaizungumzia sana.

Swali: Unatupa muda gani wa kusubiri? Pengine huoni haja ya kushirikisha jeshi la wananchi wa Tanzania?

Sirro: Siwezi kukwambia muda, huu ni upelelezi na upelelezi hauna muda. Muda wa upelelezi ni baada ya mafanikio, unajua kazi hii ni weledi, ningekuwa napanga na wale majambazi wa Ikwiriri ningekwambia muda lakini wanapanga wenyewe na mimi najipanga vizuri kuhakikisha nashughulika nao.

Kuzungumza habari ya kushirikisha jeshi, mimi sio mzungumzaji wa jeshi la wananchi lakini nnachosema, vyombo vyote tunafanya kazi kwa pamoja. Sisi wote amiri jeshi mkuu ni mmoja na mimi nazungumzia jeshi la polisi, habari ya kushughulisha jeshi la wananchi muulize CDF atalieleza.

Swali: Unawaahidi nini wananchi wa Kibiti?

Jibu: Niwahakikishie kwamba, wewe kama sio mhalifu unakimbia nini? Niwahakikishie kwamba tutashughulika na wahalifu. Wale ambao wanajua ni Raia wema ninawaomba chonde wasikimbie lakini kama kuna mtu ameonewa ndivyo sivyo tupate taarifa tupate kumshughulikia kwa sababu maelekezo tunayotoa sisi, tunashugulika na uhalifu na wahalifu. Mtu anaetumia silaha ni lazima alalamike ndugu waandishi wa habari, ukamataji unaotumika ni special. Ukamataji wake kama alivyoua askari wale wanane, ukamataji wake ni tofauti.

Raia mwema asikimbie kwani tunalipwa kwa kodi zao ila wale jamaa wanaofanya maeneo yale yasiwe na amani wakimbie sana. Lakini mawili, unapoua kwa silaha unategemea nini? Hio mtamalizia nyie wenyewe waandishi, mnaelewa nyie namna ya kumalizia.

Swali: Kuna tukio lilitokea Kurasini amabpo jeshi la polisi lilifanya shambuli na wale majambazi. Lakini baada ya pale, zimetokea tetesi nyingi kwamba alieuawa pale alikuwa ni mwananchi mwema. Kuna uwezekano polisi kwa bahati mbaya walimpiga risasi wakati alikuwa ni mwema?

Sirro: Hilo nimeshalijibu wakati nikiwa kamishina, na wewe leo nikikujibu atakuja mwengine kesho. Refer majibu yangu wakati nikiwa kamishna, majibu ni yale yale.

Swali: Kuna kesi nyingi mahakamani lakini kila ukiuliza, upelelezi haujakamilika, unaweza kulielezea! Pia waandishi wa habari wamekuwa wanapigwa na kukamatwa, wewe kama mkuu mpya wa jeshi la polisi, una kauli gani?

Sirro: Sisi ni wabia, nyinyi msipoifanya kazi yetu, msipoitangaza, najua mnawakilisha wananchi na wakati mwingine inatokea bahati mbaya. Wakati mwingine kama haujajitambulisha vizuri na umeingia maeneo ambayo kuna mapambano huwa kuna shida ya kutambua huyu ni mwandishi lakini tukishajua ni mwandishi hatuwezi kumpiga mtu ambae ni mwandishi.

Ninachosema si sahihi kumpiga mwandishi kwa sababu ni mwandishi na hata kama ni mhalifu hatutakiwi kumpiga, taratibu zinafahamika.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PADRI AUGUSTINO RAMADHANI AONGOZA IBADA YA KUMBUKUMBU YA MKE WA PROFESA SHABA DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI