IJUE BOKO HARAM KWA UFUPI


Pichani ni Ustadh Muhammad Yusuf ambaye ndiye muasisi wa Boko Haram Mwaka 2002, Boko Haram ni neno la lugha ya Kihausa lenye maana ya elimu ya Kimagharibi na neno Haram ni neno la kiarabu lenye maana ya iliyokatazwa na Mungu.

Muhammad Yusuf alizaliwa Mwaka 1970 Borno Nigeria,alipata elimu yake ya kidini nchini kwake,Chad na mwishowe katika chuo kikuu cha Madina-Saudi Arabia, Baada ya kuhitimu masomo yake alirudi Nigeria kwa ajili ya kutoa kutoa elimu kwa Umma wa Kiislam, katika Mahubiri yake mara nyingi alikuwa akiikosoa serikali yake kwa udhalimu iliyokuwa ikiufanya kwa watu wake hasa kwa watu wa Kaskazini mwa nchi hiyo, 

hali hii ikipelekea aingie katika mgogoro mkubwa na serikali ya Abuja, Mara kadhaa alikamatwa na kuachiwa, Mwaka 2009 Ustadh Muhammad Yusuf aliuawa kwa kupigwa risasi na jeshi la serikali ya Abuja akiwa mikononi mwao,

 baada ya kifo chake wafuasi wake waliandamana mjini Borno na serikali ikawauwa takribani waandamanaji 1000,baada ya mauji haya ndipo alipoibuka Aboubakar Shekau ambaye ndiye kiongozi wa Boko Haram kwa sasa, Shekau aliweza kuwavuta vijana wengi katika miji mikubwa kama Maiduguri nk kujiunga naye kuanzisha harakati za kupigana na serikali baada ya kuuawa kwa vipenzi vyao (Ustadh Muhammad na waandamanaji)

Andiko hili likupe taswira kuwa BOKO HARAM ni kundi lisilo na msimamo wa dini yoyote isipokuwa kinachofanyika ni kulipa kisasi dhidi ya serikali, Ifahamike kuwa Kabla ya kifo cha Ustadh Yusuf na waandamanaji mwaka 2009 BOKO HARAM haikuwa msituni ikiendesha mapigano kama ilivyo sasa.
Suleiman Bin Majid
LikeShow more reactions
Comment
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI

KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI