4x4

IJUE SIRI YA MAFANIKIO KTOKA WATU MASHUHURI

ma nilivyokuhaidi, kazi yangu kila Jumapili ni kukuletea nukuu kutoka kwa watu ambao wamefanya mambo makubwa au ya kipekee katika ulimwengu huu. Nukuu za leo zimelenga kukujengea uwezo au kukupa A, B, C kuelekea kwenye mafanikio yako.
Bob Brown, Roger W Babson na General Colin Powell
  1. Mtu hubeba mafanikio au kushindwa ndani yake, wala haitegemei na hali ilivyo nje – Ralph Waldo Trime.
  2. Mafanikio si funguo ya furaha, bali furaha ni funguo ya mafanikio, kama utapenda kile unachofanya utafanikiwa – Albert Schweitzer.
  3. Ikiwa ndio mara yako ya kwanza kuyafikia mafanikio, bado unatakiwa kufanya kazi kwa bidii kuendelea kusalia hapo –Richard C Miller.
  4. Weka akilini mwako, kufanikiwa au kushindwa haitoweza kuwa mwisho – Roger W Babson.
  5. Hakuna siri ya mafanikio bali ni matokeo ya kujiandaa, kufanya kazi kwa bidii na kujifunza kule uliposhindwa – General Colin Powell.
  6. Kama tuna furaha tumefanikiwa – Anna Kleirmer.
  7. Kila aliyefanikiwa nyuma yake kuna miaka mingi ya kutokufanikiwa – Bob Brown.
  8. Mafanikio ni mjumuisho wa jitihada ndogo ambazo hujirudia au kufanyika kila siku – Robert Collier.
Shukrani, dondosha comment yako hapo chini kuelezea ni nukuu ipi imekugusa zaidi.
By Peter Akaro
Post a Comment