KIONGOZI MWINGINE WA CCM AUAWA KWA RISASI KIBITI


WAKATI Taifa likiendelea kutafakari matukio ya mauaji ya kutumia silaha mkoani Pwani, mauaji mengine yametokea usiku wa kuamkia juzi.

 Mauaji hayo mapya yamemhusisha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, tawi la Njia Nne lililoko katika Kijiji cha Muyuyu, Kata ya Mtunda, wilayani Kibiti, Idd Seif aliyeuawa kwa kupigwa risasi, huku mwanaye Nurudin Idd akijeruhiwa wakiwa nyumbani kwao.

 Tukio hilo lilitokea saa mbili usiku. Mkuu wa Wilaya ya Rufiji na Kibiti ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama eneo hilo, 

Juma Njwayo amethibitisha tukio hilo. Mauaji hayo yamekuja siku nne baada ya aliyewahi kuwa katibu wa CCM kata ya Bungu wilayani humo, 

Alife Mtulia kuuawa na watu wasiojulikana ambao waliacha ujumbe kuwa marehemu alikuwa anapenda kudhulumu watu. 

Kabla ya matukio hayo, askari polisi wanane waliokuwa katika doria; Mkaguzi Msaidizi wa 
Polisi, Peter Kigugu, F 3451, k Koplo Francis, F 6990 PC Haruna, G 3247 PC Jackson, H 1872 PC Zacharia, H 5503 PC Siwale, H 7629 PC Maswi na H 7680 PC Ayoub waliuawa wilayani humo. 

Matukio ya mauaji Pwani Machi mwaka huu, polisi iliwaua kwa kuwapiga risasi watu watatu waliovalia kike wakati walipojaribu kukwepa vizuizi vitatu vya barabarani. Februari 24 mwaka huu, majambazi hayo yalimuua ofisa upelelezi, wilaya hiyo, Peter Kubezya na maofisa maliasili wawili.

 Tukio jingine ni lile la Februari 3, mwaka huu ambapo majambazi walivamia nyumba ya Mwenyekiti wa kijiji cha Jaribu, Bakari Msanga, ambaye alifanikiwa kuwatoroka. Hata hivyo majambazi hayo yalipomkosa, yalirejea na kumwaga mafuta, kisha kuichoma moto nyumba yake ambapo wakiwa na pikipiki mbili.

 Waliuawa katika daraja la Mkapa. Januari mwaka huu, katika kijiji cha Nyambunda, kitongoji cha Mkwandara, watu wasiofahamika walimuua mfanyabiashara, Oswald Mrope kwa kumpiga risasi mbele ya familia yake. Aidha, tukio lingine lilitokea Mei, mwaka jana ambapo Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambunda, Saidi Mbwana aliuawa kwa kupigwa risasi.

 Oktoba mwaka huohuo, aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Ally Milandu aliuawa baada ya kuvamiwa na watu wanne, waliompiga risasi mbili. 

Pia, Novemba mwaka jana, wenyeviti wawili wa vitongoji wa kijiji hicho waliuawa kwa kupigwa risasi. Juzi ilikuaje? Akizungumzia tukio la juzi na yaliyotangulia, Njwayo alisema taarifa alizopata ni kuwa lil
itokea majira ya saa mbili na saa tatu wakati marehemu akiwa nyumbani kwake. 

Alisema katika tukio hilo hakuna mtu aliyekamatwa, huku akibainisha kuwa wanaohusika na matukio hayo wanavizia na wanaishi na jamii, hivyo ni ngumu kuwatambua.

 “Juzi usiku tukio la mauji limetokea ambapo mzee Idd aliuwawa na mwanae Nurudini amepigwa risasa ila anaendelea na matibabu na katika uchunguzi wa awali inaonesha wauwaji wanaishi na jamii hiyo ila usiku wanatugeuka,” alisema.

 Mkuu huyo wa wilaya alisema kufuatia matujkio hayo, polisi wanaendelea na msako, huku akitolea mfano wiki iliyopita kwamba walipata taarifa kutoka kwa mwananchi kuhusu kuwepo mtu wanayemshuku kufanya matukio ya mauji na kumtia mbaroni. 

Akizungumzia katika wilaya ya Rufiji alisema wiki hii hali imekuwa shwari na polisi bado wanaendelea na operesheni. Kauli ya Jeshi la Polisi baada ya tukio Akizungumza na waandishi 
wa habari baada ya tukio la mauji wa askari, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Mssanzya alisema mauaji ya askari polisi kujirudia mara kwa mara katika maeneo hayo ya kuanzia Mkuranga, Rufiji, Ikwiriri na Kibiti ni eneo ambalo lina watu wachache, lakini kuna mapori makubwa ambayo hutoa mwanya kwa watu wenye nia mbaya kujificha. Mssanzya alisema baada ya majambazi hao kuwaua askari hao walipora bunduki saba na kutokomea kusikojulikana ambapo walifanya operesheni na kufanikiwa kutambua maficho ya muda ambapo katika majibizano ya risasi walifanikiwa kuwaua watu hao wanne pamoja na kupata silaha nne mbili zikiwa ni za askari waliouawa na mbili za majambazi hao. “Mpaka sasa nimeshapoteza askari zaidi ya 10 ninaamini wanatosha, kuanzia sasa jeshi linakwenda kwenye operesheni maalumu, hatutokuwa na mzaha, hatutokuwa na msamaha, tutakwenda kufanya kile ambacho jeshi linapaswa kufanya, tutawapata popote walipo, tutawashughulikia kikamilifu na hakuna atakayebaki,” alisema Mssanzya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*