4x4

Kwanini Mkulima Mwamwindi Alimpiga Risasi RC Dr Kleruu?


Kwa mujibu wa ushahidi wa mahakamani. ( 212. Saidi Mwamwindi v. R. Crim. Sass. 37-Iringa-72, 2/10/72. - Jaji Onyiuke)
JUMAPILI ya Krismasi, Desemba 25, 1971. RC Dr Kleruu, majira
ya alasiri, anafika Kijiji cha Ujamaa Mkungugu na nje ya nyumba ya Mkulima Said Mwamwindi.
Mkulima Said Mwamwindi akiwa kwenye trekta lake analiona gari la Kleruu limesimama nje ya mji wake. Kisha anamwona Kleruu akitembea kumfuata shambani.
Dr Kleruu anamwuliza Mkulima Mwamwindi kwa ukali, ” Kwanini unalima hapa?”
Mkulima Mwamwindi anamjibu RC Dr Kleruu;
" Nalima shamba langu".
" Shuka!"- Anaamrisha RC Dr Kleruu.
Mkulima Mwamwindi anashuka kwenye trekta.
RC Dr Kleruu anaendelea kutamka kwa ukali;
" Uwongo, shenzi".
Mkulima Mwamwindi anatamka;
" Kwanini Bwana unanitukana. Nimefanya nini?"
Naye RC Dr Kleruu anamjibu;
" Funga mdomo wako".
Kisha RC Dr Kleruu anaendelea kutamka;
" Ng'e ng'e ng'e, hi, hi, hi. Nini?"
Kisha anatamka tena;
" Tazama, ninawaambia, lakini hamsikii."
Mkulima Mwamwindi anamwuliza RC Dr Kleruu:
" Umenambia nini?"
RC Dr Kleruu anaanza kumuudhi Mkulima Mwamwindi kwa kuchanganya Kiingereza. Anasikika akitamka;
" Bloody Fool."
Wanaendelea kutembea huku RC Dr Kleruu akiwa ameshika kifimbo chake na kumtomasatomasa tumboni Mkulima Mwamwindi.
Mkulima Mwamwindi anarudi nyuma.
RC Dr Kleruu anaendelea kumtomasatomasa kwenye mapaja yake.
Mkulima Mwamwindi muda huu anaelekea nyumbani kwake huku nyuma akifuatwa na RC Dr Kleruu.
Mkulima Mwamwindi anachagua kupita njia ya mkato yenye kupitia makaburini.
Wanafika kwenye makaburi.
RC Dr Kleruu anatamka;
" Tazama, unaendelea kujenga nyumba za kudumu."
Mkulima Mwamwindi anamgeukia RC Dr Kleruu na kutamka;
" Hii sio nyumba, hapa ni mahala ninapozika ndugu zangu."
" Ni mahali unapozika mirija wenzio. Mbwa wee." Anatamka RC Dr Kleruu.
Inaendelea...
Maggid Mjengwa,
Iringa.
Post a Comment