Mabeki wa Arsenal Gabriel na Koscielny kutocheza FA


Gabriel baada ya kupata jeraha la goti katika mechi dhidi ya Everton akitolewa uwanjaniHaki miliki ya pichaISTOCK
Image captionGabriel baada ya kupata jeraha la goti katika mechi dhidi ya Everton akitolewa uwanjani
Beki wa Arsenal Gabriel hatoshiriki katika fainali ya kombe la FA siku ya Jumamosi dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Wembley baada ya kupata jeraha litakalomweka nje kwa wiki nane.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyebebwa katika machela na kutolewa uwanjani katika mechi ya ushindi dhidi ya Everton, siku ya Jumapili anauguza jeraha la goti.
Beki mwenza Laurent Koscielny pia naye hatoshiriki mechi hiyo ya fainali baada shirikisho la soka nchini Uingereza FA kukataa rufaa ya kadi nyekundi dhidi ya Everton.
Beki mwengine wa tatu wa Arsenal Shkodran Mustafi hajulikani iwapo atacheza.
Mustafi anaugua tatizo la mshtuko baada ya kupigwa kichwani wakati wa mechi dhidi ya Sunderland.
Laurent Kolscieny akipewa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Everton baada ya kucheza visivyoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLaurent Kolscieny akipewa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Everton baada ya kucheza visivyo
Katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Jumatano, mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alithibitisha kwamba Gabriel hatocheza hadi mwezi Agosti.
Aliongezea kuwa anasubiri maafisa wa matibabu kubaini hatma ya Mustafi iwapo anaweza kucheza.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MAMEYA WA TEMEKE, UBUNGO WATWANGANA UCHAGUZI WA NAIBU MEYA DAR

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

RAIS MSTAAFU KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MWANAHABARI ATHUMAN HAMISI DAR