MGALU: WANAWAKE WAUNGANE /WACHAPE KAZI KUJIINUA KIUCHUMI



Mwenyekiti wa umoja wa kikundi cha Pwani Generation Queens,wa kwanza kushoto Betty Msimbe akitoa taarifa ya kikundi kwenye uzinduzi wa kikundi hicho wa pili ni makamu mwenyekiti wa kikundi Cath Katele, ambapo mgeni rasmi alikuwa mbunge viti maalum mkoani Pwani Subira Mgalu
Mbunge wa viti maalum mkoani Pwani Subira Mgalu, akizindua umoja wa kikundi cha Pwani Generation Queens. 


Wanaumoja wa kikundi cha Pwani Generation Queens, wakisheherekea uzinduzi wa kikundi chao, uliofanyika, ukumbi wa Triple J Kibaha. (picha na Mwamvua Mwinyi) 

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

Mbunge wa viti maalum mkoani Pwani Subira Mgalu, amewataka wanawake kuacha ubinafsi /kujibweteka,badala yake wathubutu kujenga umoja na kuchapa kazi ili kujiinua kiuchumi. 

Aidha amekemea tabia ya kusemana, fitna na majungu kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha vikundi vingi kuvunjika .

Akizindua umoja wa kikundi cha wanawake wajasiriamali (Pwani generation queens),Subira alisema, wanawake ni jeshi kubwa endapo wakijidhatiti kwa kutumia fursa za maendeleo watapiga hatua zaidi. 

Alieleza kwamba, zipo fursa mbalimbali zinazoweza kuwasaidia wanawake lakini kama wataendelea kujiweka peke, fursa hizo hazitoweza kuwafikia mmoja mmoja. 

Subira alibainisha fursa mojawapo ni sanjali na kutumia taasisi ya uwezeshaji chini ya serikali -baraza la uwezeshaji la taifa. 

"Wengi hawalifahamu ,lakini taasisi hiyo inatoa udhamini kwa umoja wa vikundi,na kudhamini kukopa kwenye taasisi za kifedha ikiwemo Tanzania Posta Bank, bank ya Wanawake nchini na NMB. "alisema. 

Mbunge huyo alielezea, taasisi hizo zinatoza asilimia nafuu ambapo Tanzania posta bank wanachaji asilimia tatu. 

"Napongeza serikali kwa namna waziri wa ofisi ya waziri mkuu kuzileta pamoja taasisi za uwezeshaji, sisi wawakilishi kazi yetu kuzifuatilia, kuziletea mrejesho na kutoa elimu kwa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali viweze kuungana kwa kuandaa katiba ili vipate fursa "alisema. 

Kwa mujibu wa Subira, tayari bank kuu imepunguza riba ambayo zinatoa taasisi nyingine za kifedha hivyo anaamini taasisi hizo zitapunguza riba. 

Subira aliiomba serikali, kama ilivyochukua hatua kupitia bank kuu kuingilia kwa kupanda kwa riba kwenye taasisi za kifedha ambazo zina hisa zake ikiwemo bank ya wanawake. 

Hata hivyo alisema, amekuwa champion na muumini wa kusisitiza halmashauri kutenga asilimia tano za wanawake na asilimia tano kwa vijana. 

Aliwataka wanawake waache kujitenga bali waungane ili waweze kunufaika na fedha za halmashauri, taasisi zisizo za kiserikali na baraza la uwezeshaji. 

Awali akizindua kikundi cha Pwani Generation Queens, alijiunga na kikundi hicho kwa kuchangia sh. 100,000 .

Subira aliuomba umoja huo waache tofauti zao, wapendane ili wawe mfano katika mkoa wa Pwani na mikoa mingine.

Nae mwenyekiti wa kikundi cha malkia Pwani, Betty Msimbe, alisema kikundi hicho ni kichanga kikiwa na wanachama 100 na kinaongozwa na katiba .

Alisema wanachama wake ni kuanzia miaka 18 na kuendelea wakiwa ni wakazi wa maeneo ya wilaya ya Kibaha,Kisarawe na Ubungo .

Betty alisema, lengo la kikundi ni kushirikiana katika mipango ya kimaendeleo, shida na raha na kuwezeshana. 

Nao wanachama wa kikundi, Rehema Kawambwa, Zarina Zenzele walisema endapo watashirikiana wanaamini nia na malengo ya kikundi yatafikiwa. 

Waliomba serikali na taasisi mbalimbali za kijamii kuwaunga mkono ili waweze kuwezeshwa na kupiga hatua kiuchumi.

Mwisho 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.