MGODI WA BULYANHULU WAZINGIRWA NA POLISI

Jeshi la Polisi limeuzingira mgodi wa  Bulyanhulu baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellaack kuzuiwa kuingia katika mgodi huo alikokwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA).

Jeshi hilo limefanya hivyo baada ya Tellack kuagiza kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anyetoka wala kuingia.

Mapema leo, Mkuu huyo wa mkoa alitembelea mgodi mwingine wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia kama ulivyo ule wa Bulyanhulu.

Katika mgodi wa Buzwagi, Tellack na msafara wake waliruhusiwa kuingia na kishuhudia shughuli za uchimbaji ukiwa umeshitishwa kwa kukosekana maofisa wa TMAA walioondoka mara baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja bodi na kutengua uteuzi wa watendaji wakuu wa wakala hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI