MKUDE ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALINI, ASEMA YUKO VIZURI KABISA


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude ameruhusiwa kutoka katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam alipokuwa amelazwa tangu jana kufuatia ajali ya gari iliyotokea eneo la Dumila mkoani Morogoro.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo baada ya kutoka hospitalini hapo, Mkude alisema kwamba yuko vizuri na hana tatizo lolote ukiondoa michubuko kidogo.
“Daktari amesema ni mshituko tu baada ya ajali, lakini sijaumia popote na ninaweza kuendelea na ratiba zangu kama kawaida,”amesema.
Jonas Mkude alipokuwa hospitali ya Muhimbili kabla ya kuruhusiwa mapema leo

Mkude na watu wengine watano akiwemo dereva walikuwa kwenye Totota Land Cruiser V8 wakisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na walipofika Dumila tairi la mbele likapasuka na gari hiyo kupoteza mwelekeo hadi kwenye pori upande wa kushoto.
Abiria mmoja, Shose Fidelis alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya Mkoa wa Morooro, wakati wengine, Jasmin na Faudhia wamelazwa hospitalini hapo, huku dereva ambaye pia ndiye mmiliki wa gari ajulikanaye kwa jina la utani, Rais wa Kibamba anashikiliwa na Polisi.
Shose enzi za uhai wake kabla ya kufariki jana kufuatia ajali ya gari 
Mkude alikuwa anatoka Dodoma, ambako juzi aliisaidia Simba kukata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*