4x4

MKUDE WA SIMBA APATA TENA AJALI DAR

Gari ya Meya wa Jiji la Dar imepata ajali jana jioni  hii Jijini Dar.

Ilikuwa inapita kwenye barabara za mwendokasi na ikavaana na bodaboda.

Inadaiwa ilikuwa imembeba majeruhi Mwana Simba Jonas mkude, (wale waliovunja mpapai jana), iliyotokea huko Dumila,mkoani Morogoro ikimuwahisha Hospitali ya Taifa Muhimbili.
#Fukuzakabisabodaboda

Ujumbe wa Chadema huu hapa

Makamanda tumepata ajali, gari ya Mstahiki Meya imeharibika vibaya... Awali tulikuta ajali pale Dumila/Dakawa Morogoro, katika ajali hiyo tulikuta mtu mmoja amefariki na majetuhi watano, katika majeruhi hao tulimtambua mmoja kwamba ni Jonas Mkude mchezaji wa Simba na Timu ya Taifa, tukaamua kumchukua kwaajili ya kumpeleka Muhimbili Dar kwakuwa angalau hakuzidiwa sana,

Tulipofika Manzese Tiptop Dar tukapata ajali baada ya kumgonga mwendesha Bodaboda, hatukujeruhiwa katika ajali hili, tukalazimika kutafuta gari nyingine ili kumuwahisha mgonjwa Hospital kwakuwa gari ya Mstahiki Meya ilikuwa imeharibika vibaya,

Tumemfikisha mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu......

Na Yericko Nyerere.
Post a Comment