Mnufaika wa Airtel Fursa baada ya kupigwa tafu na Airtel Fursa

Theresia Maliatabu, mnufaika wa mradi wa Airtel Fursa akimsikiliza mteja wakati alipohudhuria maonyesho ya bidhaa na kuonyesha kazi ya uchoraji wa picha za Sanaa anazozifanya hivi karibuni.



·         Mnufaika wa Airtel FURSA bidhaa zake ziko sokoni mikoa zaidi ya mitano

Mradi wa Airtel Fursa umeendelea kufanikiwa kwa kuendelea kuwezesha vijana nchini ambapo mmoja kati ya waliowezeshwa mwaka jana Bi Threria Maliatabu  mkazi wa Mbagala jijini Dar es Saalam  ameelezea jinsi mradi huo ulivyomuwezesha kukuza kipato na kupata mafanikio ya kuanza  kujenga nyumba yake binafsi,  kujinunulia shamba la eka 2 huku akiwaasa vijana wenzake nchni na wale wote waliowezeshwa na Airtel FURSA kuchangamkia fursa hizi pindi zinapotokea.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es saalam , Bi Maliatabu ambaye anajishughulisha na biashara ya uchoraji wa picha za sanaa alisema  “ najivunia sana kuwa mmoja kati ya vijana walioshikwa mkono na Airtel Fursa kwa sababu program hii imeweza kunitoa kutoka niliopokuwa hadi kufika kwenye haya mafanikio niliyo nayo leo.  Kwakweli nimekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kuboresha kiwango cha bidhaa zangu , nimefanikiwa kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya vyumba vinne na pia nimeweza kukunua shamba la eka 2 Mkuranga mkoa wa pwani.  lengo langu ni kuanzisha shughuli za kilimo  ili kutanua wigo wa biashara yangu  lakini pia kuendelea na shughuli yangu ya  uchoraji nayoifanya kwa sasa”

Aidha Maliatabu alifafanua kuhusu changamoto mbalimbali katika biashara ikiwemo masoko ya nje , usafiri wa kusambaza bidhaa zake huku akieleza kuwa baadhi ya changamoto hizi ameshaanza kuzishughulikia  na kuomba wadau mbalimbali kuweza kumsaidia.

“Nimeweza kuongeza masoko yangu na kufikia masoko ya Zanzibar, Moshi , Arusha na Dar, na kwa sasa niko katika mchakato wa kupeleka bidhaa zangu nchini Sweeden na Italy. Mipango hii ikikamilika kwakweli nitakuwa nimefurahi kufikia malengo yangu na naamini nitafanya vizuri zaidi na kukuza kipato changu zaidi. Natoa wito kwa vijana wenzangu kujituma na kufanya kazi kwa bidiii na kutafuta fursa mbalimbali na kujikita kwenye ujasiriamali badala ya kusubiri ajira ambazo zimekuwa ni changamoto”.

Akiongea kuhusu mafanikio haya, Meneja Huduma kwa Jamii, Bi Hawa Bayumi alisema ,  tunafarijika na kujisikia fahari kuona jinsi gani program hii imeweza kuwainua vijana hawa wajasiriamali wenye nia ya kukuza kipato na kufikia malengo yao. Theresia Maliatabu ni mfano wa kuigwa, alipowezeshwa alijiongeza na kufanya kazi kwa juhudi kubwa na maarifa. Nawaasa vijana wajitume na kuchangamkia fursa kama hizi zinapojitokeza wazitumie vizuri ili kuleta tija kwenye maisha yao, familia zao na taifa kwa ujumla.”
                                                                                                                                                                                                
Theresia Maliatabu ni moja kati ya vijana waliochagulia kuwa kati ya wafanyabiashara wadogo wadogo watakaonufaika na mpango wa Airtel FURSA  na kupatiwa vitendea kazi zikiwemo , ubao wa kuchorea, vifaa vya kuchorea na computer, mafunzo ya ujasiriamali na kutengenezewa kipindi maalumu cha Television kilichoonyesha safari yake katika biashara ambavyo vimemsaidia kukuza biashara yake. Airtel  kupitia mpango wake wa Airtel fursa imewezesha vijana takibribani 5000 kwa kuwapatia mafunzo ya ujasirimali na baadhi yao kupata vitendea kazi ili kuboresha biashara zao.

Mwisho


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA