Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya Itel, Cooper Chen akimtambulisha rasmi msanii maarufu wa filamu za Tanzania ‘Bongo Movies’ Irene Uwoya (kushoto) kuwa barozi wa itel Mobile Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa Habari wa kampuni hiyo, Wolle Fernando na Ofisa Masoko Itel Dar es Salaam, Asha Mzimbili. (NA MPIGAPICHA MAALUMU)
Wakitiliana saini mkataba
Wakitiliana saini mkataba
Abraham Ntambara
KAMPUNI ya Itel imemtamburisha rasmi
msanii maarufu wa filamu za
Tanzania ‘Bongo Movies’ Irene Uwoya kuwa
barozi wa itel Mobile Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia jana.
Akizungumza wakati wa jutambulisho
huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam Ofisa Habari wa Itel nchini Wolle
Fernando, alisema kupitia umaarufu alionao msanii huyo ni imani kwao kuwa
ataweza kushiriki nao vyema katika shughuli za kijamii.
“Irene ni msanii maarufu, tunaamini
kupitia yeye ataweza kuunganisha itel mobile na watanzania kwa ujumla wao,”
alisema Fernando.
Aidha alisema ni matarajio yao kuwa
jamii itanufaika kwa kupata elimu kuhusu bidhaa zao kupitia kwake ambapo
watasaidiana nae kwenye matukio ya kuonesha ukarimu kwa baadhi ya makundi ya
jamii ambayo wanaendesha kupitia charity event programs na mengine.
Alibainisha kuwa wanatambua mchango
wa Uwoya katika jamii kwani amekuwa akielimisha kupitia movie zake, hivyo kwa
kutambua umuhimu wake watashirikiana kikamilifu kuhakikisha jamii inapata
inachotarajia kutoka kwao.
Irine Uwoya alisema atashirikiana na
kampuni hiyo vizuri katika shughuli mbalimbali za kijamii ili kuhakikisha jamii
inafaidika kupitia charity programs na matukio mengine yanayofanywa itel.
“Nashukuru kwa kupata nafasi hii,
nitashirikiana nao vizuri, ntahakikisha kupitia nafasi hii naisaidia jamii
yangu ya Tanzania,” alisema Uwoya.
mwisho
Comments