Mwanamke, Diane Rwigara, ametangaza rasmi kugombea nafasi ya Urais Rwanda



                                                                                      Diane Rwigara
Huyu ni Binti wa mfanyabiashara maarufu wa Kinyarwanda, Assinapol Rwigara aliyefariki miaka 2 iliyopita, ana umri wa miaka 35.
Mgombea huyo wa kiti cha Urais amesema anataka kukomesha uonevu na kuleta haki na uhuru wa watu kujieleza nchini Rwanda.
Akiongea na  waandishi wa habari, Bi Diane Rwigara amesema lengo la mkutano huo ni kutangaza rasmi nia yake ya kugombea kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwezi wa 8 mwaka huu huku akieleza sababu zinazomfanya kupigania kiti hicho.
”Kuna suala la usalama mdogo ambapo baadhi ya watu hutoweka na wengine kuuawa katika mazingira ya kutatanisha. Huwezi kusema kwamba uko katika nchi yenye amani na usalama wakati watu wanauawa huku wengine wakikimbia nchi,” alisema.
Ameongezea kwamba Rwanda hakuna uhuru wa watu kutoa maoni yao na ni tatizo kubwa kwa wakosoaji wa serikali, masuala ambayo yeye anataka kubadilisha nayo.
”Siasa isiyobagua kabila au tabaka fulani, ambayo inatoa fursa kwa kila Mnyarwanda na kumpa uhuru wa kutoa maoni yake. Nataka kuondoa dhana kwamba mtu akiwa na msimamo tofauti na serikali basi ataitwa adui wa taifa, hiyo nitaipiga vita katika uongozi wangu,” alisema Bi Rwigar

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.