Ndege za China zazuia ndege ya Marekani


Ndege za China zaizuia ndege ya MarekaniHaki miliki ya pichaAFP
Image captionNdege za China zaizuia ndege ya Marekani
Ndege mbili za kijeshi za China zimeizuia 'vibaya' ndege ya Marekani kulingana na jeshi la Marekani.
Ndege hiyo inayohusika na kufanya uchunguzi, ilikuwa katika safari yake ya kutaka kugundua mionzi katika anga ya kimataifa iliopo mashariki mwa bahari ya China.
Ndege hiyo ilikuwa imetumiwa kugundua ushahidi kuhusu majaribio ya kinyuklia ya Korea Kaskazini.
China imekuwa ikituhumu vitendo vya Marekani karibu na maji hayo yenye utajiri mkubwa yaliopo katika pwani yake ,hatua ambayo imesababisha wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili.
''Swala hilo linaangaziwa na China kupitia njia mwafaka ya kidiplomasia mbali na zile za kijeshi'', msemaji wa jeshi la angani la Marekani Luteni kanali Lori Hodge amesema.
''Uzuizi huo haukufanywa kwa njia ya ''utaalamu'' kutokana na hali ya rubani wa ndege hiyo ya China ikiwemo kasi ya ndege zote mbili'', aliongezea akisema uchungzi wa kijeshi unaendelea.
Bahari hiyo ya kusini mwa China
Image captionBahari hiyo ya kusini mwa China
Mnamo mwezi Februari , ndege moja ya Marekani ilianza kile Washington ilielezea kuwa doria yake ya kawaida kusini mwa bahari ya China ikiandamana na idadi fulani ya meli za kijeshi.
Ndege na meli hizo zilielekea katika eneo hilo licha ya onyo kutoka China dhidi ya kutoa changamoto yoyote kwa uhuru wa China katika eneo hilo.
Kwa nini bahari hiyo ya kusini mwa China inazozaniwa?
Mnamo mwezi Mei 2016 ndege mbili za kijeshi za China zilizuia ndege nyengine ya Marekani iliokuwa katika anga ya kusini mwa bahari ya China.
Wakati huo, jeshi la Marekani lilisema kuwa ilikuwa ikipiga doria ya kawaida katika eneo hilo.

Mada zinazohus

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI