Ndege za kuangusha mabomu za Marekani zapaa Korea


Ndege za kuangusha mabomu aina ya B-1B Lancer zikipaa juu ya Korea Kusini awaliHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionNdege za kuangusha mabomu aina ya B-1B Lancer zikipaa juu ya Korea Kusini awali
Maafisa wa Korea Kusini wamesema ndege mbili za Marekani za kuangusha mabomu zimepaa juu ya anga la rasi ya Korea.
Ndege hizo za kivita zilipaa angani kama sehemu ya juhudi za kuzuia vitisho na uchokozi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Ndege hizo aina ya B1-B zilishiriki operesheni ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini.
Kupaa kwa ndege hizo kumetokea wakati ambapo Rais Trump ametoa taarifa za kukanganya kuhusu msimamo na sera ya Marekani dhidi ya Pyongyang.
Bw Trump aliambia Fox News kwamba msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu mpango waker wa kufanyia majaribio makombora ya nyuklia ni wa kukera.
Alikuwa awali amesema kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un, iwapo kutakuwepo na mazingira mahsusi.
Hata hivyo, msemaji wa ikulu ya White House alisema baadaye kwamba mazingira kama hayo, yanayoweza kufanikisha mkutano wa Trump na Kim hayapo.
Korea Kaskazini imeongeza kasi katika majaribio yake ya makombora na silaha za nyuklia miaka ya karibuni licha ya marufuku ya Umoja wa Mataifa.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Han Song-ryol aliambia BBC awali kwamba Korea Kaskazini inaamini kwamba silaha zake za nyuklia zinaweza "kuilinda" dhidi ya tishio la shambulio la kijeshi kutoka kwa Marekani.
Korea Kaskazini inahofia kwamba Marekani na Korea Kusini wanaweza kutumia nguvu kumuondoa madarakani Kim Jong-un.
Jumatatu, Japan ilituma meli ya kubwa zaidi ya kivita baharini, hatua yake ya kwanza ya aina hiyo tangu kupitishwa kwa sheria mpya yenye utata iliyowezesha taifa hilo kuanza kupanua uwezo wa jeshi lake.
Meli hiyo kubwa ya kubeba helikopta ambayo imepewa jina Izumo ilitumwa kuifuata meli ya kubeba mizigo na vifaa vya kijeshi ya Marekani ambayo inapitia katika maeneo ya bahari ya Japan.
Meli hiyo ya Marekani inaelekea kufikisha mafuta kwa meli nyingine za taifa hilo zinalohudumu eneo hilo, ikiwemo meli yake kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson na meli zinazoandamana na meli hiyo karibu na rasi ya Korea.
Izumo ndiyo meli kubwa zaidi ya kivita ya JapanHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionIzumo ndiyo meli kubwa zaidi ya kivita ya Japan
Korea Kaskazini imetishia kuizamisha Carl Vinson pamoja na nyambizi ya Marekani, huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka eneo hilo.
Aidha, taifa hilo lilifanya jaribio la kurusha kombora ambalo lilifeli Jumapili, licha ya kuonywa mara kadha na Marekani na nchi jingine dhidi ya kufanya majaribio ya makombora au majaribio ya silaha za nyuklia.
Kutumwa kwa Izumo kumejiri baada ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyofanywa na Japan na Marekani, pamoja na shughuli nyingine za majeshi ya majini.
Meli ya kutekeleza mashambulio baharini ya Ufaransa iliwasili kusini magharibi mwa Japan Jumamosi kwa mazoezi ambayo yatashirikisha majeshi ya majini ya Japan, Marekani na Uingereza.
Ukubwa wa meli za kivita za mataifa yenye nguvu
Image captionUkubwa wa meli za kivita za mataifa yenye nguvu
Meli kubwa ya kubeba ndege ya Marekani ya Carl Vinson ikiwa kusini mwa Japan JumamosiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli kubwa ya kubeba ndege ya Marekani ya Carl Vinson ikiwa kusini mwa Japan Jumamosi

Mada zinazohusiana

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PADRI AUGUSTINO RAMADHANI AONGOZA IBADA YA KUMBUKUMBU YA MKE WA PROFESA SHABA DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI