SHAKA AWATAKA VIJANA KUCHAGUA VIONGOZI IMARA,SHUPAVU NA WACHAPAKAZI


Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Mpanda

Na Mwandishi Wetu, Katavi

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi umesema wakati huu chama na jumuiya zake kukiwa katika hekaheka za uchaguzi kimewataka wanachama kujitokeza  waaamue kidemorasia kumchagua kiongozi yeyote mwenye sifa na anayefaa. 

Pia umoja huo imeelezea kuwa kila mwanachama ana haki ya kuchukua fomu na kuwania nafasi  ambayo anafikiri ana uwezo nayo katika kuwatumikia wananchma na chama kwa bidii na maarifa. . 

Shaka alitoa matamshi hayo jana wakati akizumgumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa uliofanyika kwenye ofisi za ccm wilaya ya  Mpanda mkoani hapa .

Alisema kazi ya siasa ni ya kujitolea hivyo kila mwanachama anayechukua fomu kutaka kuwania nafasi yoyote atambue chama kinahitaji mtu mwenye juhudi , bidii na utii ili akijenge, kukitumikia na kukitetea kwa nguvu na hekima. 

"Huu ni wakati muafaka  wa kuwapa nafasi wanachama wetu katika ngazi zote kuamua nankuchagua kwa ridhaa yao, kuwapa viongozi  kwa hiari bila kushawishiwa kwa sababu za kujongwa , rushwa, ahadi au siasa za hadaa "Alisema Shaka. 

Aidha akizungunza ziara za viongozi wa chama na jumuiya mkoani na wilayani, alisema ziara hizo ni chama , viongozi wanapita ili kutazama uhai wa chama na maendeleo yake.

Shaka alisema anapokuja kiongozi wa chama katika mkoa husika jumuiya zote zinapaswa kushiriki katika hatua za maandalizi, kupanga na kushiriki  toka mwanzo hadi mwisho .

"Ziara zote ni za CCM,CCM ina junuiya zake, jumuiya ni watoto wa chama , chama chetu ni mfano wa mti wenye mizizi mirefu , matawi makubwa yanayotoa matunda , chama na jumuiya zake wote watoto wa mtu mmoja "Alieleza .

Kaimu huyo Katibu Mkuu alisems kazi za chama na jumuiya zake ni kuhakikisha uhai wa chama unaimarika, kuongeza idadi ya wanachama wapya  na kufanya kazi kwa bidii ili kihinde na kuongoza doka.

"Tuendelee na kazi ya kukipa uhai chama chetu, wsnanchi wanakiamini, wanakiamini na hawaoni chama mbadala nje ya ccm.,wajibu wetu ni kuwasemea  wananchi katika matatizo ysnayowakabili "Alisistiza Shaka
  kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akifungua Shina la wakereketwa la mafundi baiskeli kata ya Majengo wilayan mpanda
  kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akipiga ngoma ya NSIMBA na kikundi cha wa mama Nsimba
 Wanachama wa CCM Wilaya ya Mpanda wakishangilia katika Mkutano wa Ndani Wa kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka.
 Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa Haidar Sumri akizungumza katika mkutano wa Ndani Wa kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka.
  kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiagana na wananchi mara baada ya kumaliza Mkutano wa Ndani katika wilaya ya Mpanda Mkoani katavi.
  kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akitoa jezi katika timu zilizo shinda kombe la MBOGO CUP kwa ufadhili wa Mbunge jimbo la Nsimbo.
  kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akikagua Mradi wa  kilimo cha bamia wa Vijana wa kavicha uliopo kata ya kasokola wilayani mpanda picha na (FAHADI SIRAJI)
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA