SIMBA WATINGA NA KOMBE BUNGENI DODOMA

 Viongozi na wachezaji wa Simba wakiwa bungeni Dodoma leo
 ​Wachezaji wa Simba wakiwa na wabunge wapenzi wa timu hiyo walipokwenda na Kombe la Ubingwa wa Shirikisho bungeni Dodoma

Dodoma. Siku moja baada ya klabu ya Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho, imepata mwaliko bungeni.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza, bao lililopatikana ndani ya dakika ngumu 120 katika mchezo uliopigwa jana Jumamosi makao makuu Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Kwa matokeo hayo, Simba imekata tiketi ya kupanda ndege na kuungana na watani zao Yanga. Simba watawakilisha Taifa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Pia, baada ya kupeleka kombe hilo bungeni, itakwenda Kondoa kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki na Kondoa Kombaini.

Baada ya kukamilisha ratiba hiyo, itasafiri kwa basi kurudi Dar es Salaam tayari kujiandaa na mashindano ya Ligi ya Sportpesa.

Chanzo: Mwananchi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI