SIRRO ASEMA ILIKUWA SAHIHI POLISI KUMUUA 'JAMBAZI' ATM KURASINI

Abraham Ntambara
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro, amesema jeshi hilo lilikuwa sahihi kumuua kijana aliyetuhumiwa kwa ujambazi wa kutaka kupora fedha zilizokuwa zikisambazwa katika ATM za tawi la benki ya CRDB Kurasini hivi karibuni.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema jeshi hilo halipo kwa ajili ya kumuonea mtu hivyo kitendo  hicho kilitokea kwenye tukio na kwamba hakufuatwa nyumbani kwake.
“Kimsingi kama kuna mtu anashaka na hilo upelelezi upo umefanyika, warudi kwenye eneo la tukio wakaulizie, kama ni mtu mwema alapoambiwa asimame angefanya hivyo na kunyanyua mikono juu, lakini hakufanya hivyo bali alikuwa akimfuata askari,”
“Sasa ulitaka askari afanye nini akimbie?, waende pale wakaulize, watu wapo tumewauliza na wametueleza mambo ambayo amekuwa akifanya yule kijana, sisi hatupo kumuonea mtu, ni kutenda haki, ukiingia kwenye laini yetu ya uhalifu tutakushughulikia kwa mujibu wa sheria,” alisema Sirro.
Aidha alisema amekuwa akiona malalamiko kwamba kijana huyo alikuwa mwanafunzi mzuri, anafundisha Madrasa pamoja nakufundisha online ambapo aliwataka wananchi kukumbuka kuwa mazingira ambayo mauaji yalifanyiak yanafahamiaka kutokana na nikutokana na kwamba kulikuwa na fedha ambazo zilitaka kuporwa.
Alisema hata kama mtoto wako kama ni muharifu hawezi kukuambia, aukuwa mwalimu wa madrasa ndiyo huwezi kuwa mharifu
Kamshina Sirro alisisitiza kuwa watu kusema hakuwa jambazi siyo siyo sahihi kwani suala hilo ni lakiupelelezi na upelelezi ndiyo unaoweza kulibaini hilo.
Mei 14 mwaka huu Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam katika eneo la Kurasini kwenye jengo la Mako Makuu ya Uhamiaji lilifanikiwa kumuua kwa risasi mtu aliyesadikiwa kuwa ni jambazi akijaribu kumnyang’anya silaha askari aliyekuwa akisindikiza gari la kampuni ya G4S lililokuwa limebeba fedha Tsh. 320,000,00 zilizokuwa zikisambazwa kwenye ATM za Benki ya CRDB.
Aidha baada ya tukio hilo kuna taarifa za ndugu na jamaa wamarehemu walijitokeza na kukanusha kuwa ndugu yao hakuwa jambazi.

mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA