STAR TIMES YAINGIA UBIA NA TPB KUUZA LUNINGA KWA MKOPO

Mkurugenzi wa Operesheni na Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Jema Msuya wa kwanza kulia na Makamu wa Rais wa Kampuni ya StarTimes nchini Zuhura Hanifu wakikata utepe katika hafla jana jijini Dar es Salaam ambapo Kampuni ya StarTimes imeingia ubia na TPB kwa lengo la kuwakopesha wateja televisheni za kidigitali kwa awamu kupitia mkopo ambao utamwezesha kulipa ndani ya mwaka mmoja kutoka benki hiyo.(PICHA NA Abraham Ntambara)

Abrahm Ntambara
KAMPUNI ya StarTimes imeingia ubia na Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa lengo la kuwakopesha wateja televisheni za kidigitali kwa awamu kupitia mkopo ambao utamwezesha kulipa ndani ya mwaka mmoja kutoka benki hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuingia katika ubia huo, Makamu wa Rais wa Kampuni ya StarTimes nchini Zuhura Hanifu, alisema hiyo ni njia rahisi itakayomsaidia mteja wao kulipia televisheni yake kwa awamu.
“Wateja wataweza kuipata huduma hii katika mikoa mitano, Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha na Mbeya ambapo kuna matawi ya benki hiyo,” alisema Hanifu.
Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Antony Katunzi alisema, “Ushirikiano huu unaashiria wazi mapindizi ambayo benki na kampuni ya televisheni zinaweza kuleta, kwa kurahisisha ulipaji kwa wateja wao na jamii kwa ujumla ili kuwezesha kila familia kumiliki luninga ya kidigitali ya StarTimes,”.
Meneja Masoko wa TPB alisema benki hiyo imekubaliana na StarTimes kutoa mikopo hiyo midogo kwenye mikoa mitano amabayo inapata huduma za benki hiyo.
Alisema katia hatua hiyo wateja wasio wa kampuni hyo wanaweza pia kulipia luninga hizo kwa awamu kupitia matawi yote ya TPB, waishio mijini na vijijini wataweza kupata luninga kwa urahisi kulingana na mahitaji yao.
Naye Mkurugenzi wa Operesheni na Teknolojia wa TPB Jema Msuya alisema kuwa kwa awamu ya kwanza wataanza kutoa huduma ya mikopo hiyo kwa wafanyakazi wa Taasisi za serikali pekee.
Aidha alieleza kuwa watakao hitaji mikopo hiyo wakifika benki watashughulikiwa nadani ya siku tatu na kisha kupata mikopo hiyo ambapo wataenda katika madoka ya StarTimes na kupatiwa luninga.
Luninga hizo za kidigitali zimetolewa katika matoleo mbalimbali ili kuendana na wateja kulingana na mahitaji na uwezo wao. Zilitajwa luninga hizo kuwa ni inchi 24 kwa sh.45000, inchi 32 kwa sh. 64000 na inchi 40 kwa sh.99000.
mwisho


0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA