Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) na Mkurugenzi wa Startimes, Wang Xiaobo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk. Ayub Rioba wakionesha mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 20 zilizochangwa kwa ajili ya kuisaidia timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17 Serengeti Boys katika hafla iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Startimes Juma Suluhu. (PICHA NA ABRAHAM MTAMBARA)
Abraham Ntambara
KAMPUNI ya Star Media Tanzania imekabidi hundi ya sh. milioni 20 kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Dk.Harisson Mwakyembe katika harambee iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ya kuchangia timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inayojiandaa kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa StarTimes Tanzani Wang Xiaobo, aliwatakia vijana hao kila la kheri ili iweze kuliwakilisha vyema Taifa katika ulimwengu wa michezo.
“Tunafuraha kubwa sana kuichangia Serengeti boys pamoja na serikali katika jitihada za kukuza michezo nchini,Tunaitakia timu kila la kheri iweze kuwakilisha vema nchi katika medani za kimichezo”
Aidha alieleza kuwa mafanikio ya michezo kwa baadae yanategemea msingi mzuri na uwekezaji kwa vijana kwani ni hazina nzuri na tegemeo la kesho kwa kuliletea mafanikio taifa.
Alibainisha kwamba, mbali na uchangiaji huo wataendelea kuchangia katika michezo mingine pamoja na shughuli za kiuchumi na kijamii ili kuisaidia nchi katika jitihada zake za kuleta maendeleo kwa wananchi.
Waziri wa Habari,Utamaduni , Sanaa na Michezo Dk. Mwakyembe aliishukuru kampuni hiyo kwa mchango wake na kuahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kufanikisha malengo yao na pia michezo kwa ujumla .
"Nawashukuru sana kwa mchango huu, nawahakikishia serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kufanikisha malengo yake," alisema Dk. Mwakyembe
Pia, aliongeza kuwa bado sekta ya michezo inakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini wizara yake itaendelea kurekebisha ikishirikiana na wadau wengine ili kuleta mabadiliko katika sekta hii.

Comments