TLS YAKABIDHI MSAADA WA VITABU 20 KWA WASIOONA


Ofisa Elimu Maalum Wilaya Ilala, Salehe Msechu wa pili kutoka kulia akionesha kitabu cha nukta nundu, katika hafla ya kukabidhi vitabu 20 vya nukta nundu  kwa ajili ya wanafunzi wasioona katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Madeline Kimei, akifuatiwa na Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wasiona Tanzania, Jonas Lubago na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana. (PICHA NA SULEIMAN MSUYA) 

Suleiman Msuya

JUKWAA la Haki na Usalama linatarajia kugawa vitabu 7,000 ambavyo vimebeba ujumbe kuhusu mambo 101 mwananchi anapaswa kuyajua kuhusu polisi huku vitabu 300 vikilenga watu wenye mahitaji maalum.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Madeline Kimei wakati akizindua na kukabidhi vitabu 20 vya nukta nundu kwa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam jana.

Alisema TLS imejipanga kugawa vitabu hivyo ambayo vitasaidia jamii ambayo imekuwa ikikutana na changamoto mbalimbali wakati ikikutana na polisi.

Kimei alisema TLS kwa kushirikiana na Jukwaa la Haki na Usalama imeweza kuandaa machapisho manne yanayohusu polisi ambapo mawili ni nyaraka za majadiliano ambayo inahusu uhuru wa kioperesheni na uwajibikaji wa jeshi hilo.

Alisema mengine mawili ni vitabu vya kutoa uelewa kwa wananchi juu ya polisi na mbaraza ya usalama ya wilaya ambapo mwitikio umekuwa mkubwa.

“Siku ya leo tuko hapa kwa ajili ya kuzindua toleo la nukta nundu la moja wapo ya vitabu vilivyochapishwa chini ya mradi huu ambapo kitabu hiki kinaitwa “mambo 101 unayoyahitaji kuyafahamu juu ya polisi lakini unaogopa kuyauliza,” alisema.

Mjumbe huyo alisema uandaaji wa vitabu vya nukta nundu unagharama kubwa lakini kutokana na wao kutambua umuhimu wa kundi hilo wamelazimika kuchapisha vitabu 300 kwa kuanzia katika kundi hilo.

Alisema lengo kuu ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wantambua kazi za polisi jinsi zinavyofanywa na changamoto ambazo wanakutana nazo.


Kimei alisema kitabu hicho kitaelimisha jamii jinsi jeshi hilo linavyofanya kazi na ukomo wake wa madaraka hivyo kila pande kutekeleza majukumu yake kwa haki.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo Ofisa Elimu Maalum Wilaya ya Ilala, Salehe Msechu alisema uamuzi wa Jukwaa la Haki na Usalama ni wa kuungwa mkono na jamii huku akisisitiza wadau wengine kujitokeza kusaidia.

Msechu alisema Serikali imejipanga kusaidia kundi la watu maalum hivyo itajitahidi kutoa vifaa mbalimbali ambavyo vitatumika kwa wanafunzi katika wilaya hiyo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mchanganyiko, Anna Msechu alisema shule hiyo ina wanafunzi 69 wasiona hivyo vitabu hivyo vya nukta nundu vitasaidia kuatua tatizo.

“Hapa nina wanafunzi 69 ambao watafaidika na vitabu hivi havikidhi hitaji lakini vitasaidia kwa kiasia fulani tunaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia,” alisema.

Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wasiona Tanzania, Jonas Lubago alisema vitabu vya watu wa elimu maalum hasa wasiona kwa Tanzania vinapatikana kwa chini ya asilimia mojo hivyo jitihada zinahitaji ili kukidhi hitaji.
Mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI