Trump anakutana na Papa Francis Vatican


Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump waliwasili Roma JumanneHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRais Donald Trump na mkewe Melania Trump waliwasili Roma Jumanne
Rais Donald Trump anatarajiwa kuzungumza na Papa Francis na viongozi nchini Italia mjini Roma katika awamu ya tatu ya ziara yake baada ya kuingia madarakani.
Trump na kiongozi huyo wa kidini tayari wame tofautiana kiasi kuhusu masuala yakiwemo uhamiaji na mabadiliko ya tabia nchi.
Kiongozi huyo wa Marekani anakutana pia na rais wa Italia na waziri mkuu, kabla ya kuelekea Brussels kwa mkutano wa jumuiya ya kujihami NATO.
Awali aliapa kufanya kila awezalo kuisaidia Israel na Palestina kuidhinisha amani alipokamilisha ziara yake mashariki ya kati.
Pope Francis.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionPapa Francis ameshutumu hatua ya rais Trump kujenga ukuta katika mpaka baina ya Mexico na Marekani
Papa Francis na Rais Trump ni viongozi wawili walio na tofauti kubwa.
Upande mmoja Papa ameelekeza maisha yake kutetea maskini na wasiojiweza na upande mwingine mfanyabiashara, Rais Trump amelenga kutajirika na amejihusisha na mabilionea katika baraza lake la mawaziri.
Na licha ya kwamba huu utakuwa mkutano wao wa kwanza, tayari wametofuatiana. Wakati wa uchaguzi, na katika ziara yake katika mpaka wa Mexico na Marekani, Papa Francis amesema watu wanaofikiria tu kujenga ukuta badala ya madaraja sio wakristo.
Donald Trump amesema matamshi hayo ni ya kuaibisha na amemshutumu kiongozi huyo wa kidini kwa kuwa kibaraka cha serikali ya Mexico.
Lakini leo Jumatano wote watapania kuelewana.

Mada zinazohusiana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*