Vijue vigezo vya kupata kazi Usalama wa Taifa


Taasisi za Usalama wa taifa ni moja ya taasisi nyeti kwenye taifa lolote duniani ambapo tukiwa nje huwa tunasikia au kuambiwa kwamba wanaofanya kazi humo ni watu wenye mafunzo maalum na huwa hawajionyeshi au kujitangaza kwa watu kuhusu wanachofanya.
Leo millardayo.com na AyoTV zinae Evarist Chahali, Mtanzania anaeishi Ulaya lakini pia anasema aliwahi kufanya kazi kwenye Idara ya usalama wa taifa zamani lakini kwa sasa amestaafu.
Chahali ameandika kitabu kiitwacho SHUSHUSHU ambapo anasema ‘moja ya mahitaji makubwa ya mtu kupata kazi hii ni kutakiwa kuwa na akili ya ziada na sio akili ya kawaida tuliyozoea ambapo upatikanaji wa watu wa aina hii hupitia hatua mbalimbali’
Naomba ieleweke kuwa kwenye kitabu hiki sijazungumzia Idara ya usalama wa Taifa Tanzania bali nimezungumzia Idara za usalama wa taifa kote duniani kwani taaluma hii inafanana kama ilivyo Udaktari na taaluma nyingine
Kitabu kinazungumzia changamoto pia, kimsingi huko nyuma kwenye miaka ya 80 na 90 mwanzoni changamoto kubwa kwenye idara za usalama wa taifa ilikua wenyewe kwa wenyewe, yani idara ya nchi moja dhidi ya idara ya nchi nyingine… kulikua kama kuna kanuni flani zinatakiwa kuheshimiwa japo sio rasmi
Tishio kubwa kwa sasa kwa Idara za Usalama wa taifa duniani ni ugaidi wa kimataifa unaochangiwa na mwamko wa kidini wa makundi kama AL SHABAAB, ISIS, AL QAEDA na wengine…. hawa pia wanatumia Ushushushu lakini hawafuati kanuni
‘Nina malengo makubwa mawili yaliyofanya niandike hiki kitabu, kwanza ni kuondoa dhana potofu kuhusu taaluma hii kwamba kuna watu wanasema hawa ni Wanyonya damu, Wananyonga na kung’oa kucha, kitabu hiki hakizungumzii Idara ya usalama wa taifa Tanzania bali kinazungumzia taaluma hii duniani kwa ujumla’ – Evarist Chahali
Ukitaka kukisoma kitabu hiki unaweza kuingia chahali.com Amazon UK search SHUSHUSHU @chahali au kwa Tanzania unaweza kupiga 0717 331 444.
UNAWEZA KUMSIKILIZA EVARIST KWA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI

EXCLUSIVE: Meya aliyezuiwa na USALAMA WA TAIFA kuingia kwenye kikao alipo Rais Magufuli aongea, BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*