WANANCHI WA KITETO WAENDELEA KUJIUNGA NA MFUKO WA PPF


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera (wa pili kulia) akikabidhiwa vifaa tiba na Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Bi. Lulu Mengele (wa pili kushoto) kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Kiteto katika hafla iliyofanyika mwishoni wa wiki iliyopita. PICHA NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG- KITETO. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera akitoa maelezo mafupi kuhusu faida za kujiunga na Mfuko wa PPF katika hafla ya kukabidhiwa vifaa tiba toka Mfuko wa PPF kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Kiteto, Manyara. Mkuu wa wilaya Kiteto, Manyara, Bw. Tumaini Magesa akitoa shukrani zake za pekee kwa Mfuko wa PPF jinsi ilivyoweza kuwakomboa wananchi wa wilaya yake kwa kuwapatia vifaa tiba. Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini, Bw. Jacob Sulle akiendelea kutoa elimu kwa wananchi wa wilaya ya Kiteto, Manyara ili waendelee kujiunga na Mfuko wa PPF. Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Bi. Lulu Mengele akitoa maelezo mafupi wakati wa ugawaji wa vifaa tiba vilivyotolewa na PPF katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto.   Makamu Mwenyekiti wa Wilaya ya Kiteto, Bw. Paul Tunyoni akitoa shukrani zake za pekee kwa Mfuko wa PPF kwa kuweza kuwafikia wananchi wengi na kuwapa elimu juu ya kujiwekea mafao kwa mfumo wa 'WOTE SCHEME'.
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya Kiteto walioweza kuhudhuria halfa ya ugawaji wa vifaa Tiba.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera akimkabidhi kitambulisho cha uanachama wa Mfuko wa PPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari 'WOTE SCHEME' kwa Mfugaji Ngaisi Laizer. Mfugaji Ngaisi Laizer akionesha kitambulisho chake cha uanachama wa mfuko wa PPF.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa PPF na viongozi wa wilaya ya Kiteto.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Bi. Janet Ezekiel akiwaandikisha wanachama wapya wa Wilaya ya Kiteto, Manyara. Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini, Bw. Jacob Sulle (wa kwanza kulia) akiwaandikisha wanachama wapya wa Wilaya ya Kiteto, Manyara.   Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kiteto wakijiunga na Mfuko wa PPF baada ya kupata elimu.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Bi. Lulu Mengele akitoa elimu kwa wananchi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU