Watu walalamika rambirambi kuchepushwa


Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Thomas Ngawaiya alisema malalamiko hayo mengi yalikuwa ni yale ya watu waliyopata maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera na rambirambi za wanafunzi 32 wa shule ya Lucky Vincent iliyopo Arusha, waliyopata ajali ya gari.
Ngawaiya alisema watu wanalalamika fedha zao kwenda kutengeneza barabara, bila kujali kuna watu wameumia na wanahitaji msaada wa kuwavusha pale walipo kutokana na matatizo waliyoyapata.
Alisema Serikali inatakiwa iliangalie suala hili kwa jiko la pili la huruma kwa sababu watu wamekata tamaa, kutokana na kwamba wanajitoa kwa moyo wote kuchangia fedha kwa watu waliyopata matatizo halafu zinakwenda kufanya mambo mengine jambo ambalo si jema.
“Watu wamekata tamaa kwa sababu wanajitolea fedha nyingi ili ziende kwa walengwa, lakini hazifiki na mwisho wa siku wafiwa ndiyo wanaingia gharama, wakati Serikali ilikuwa na bajeti yake,”alisema Ngawaiya.
Alibainisha kuwa kama mambo haya yataendelea hivi watu watashindwa kujitoa, kwa sababu wao wanatalaji msaada uende kwa walengwa, lakini hazifiki ambapo kiutawala bora si sahihi kufanya jambo kama hilo.
Alisema kinachotakiwa kufanywa na Serikali ni kuwahesabu watu waliyopatwa na matatizo hayo na kugawa michango, ndiyo maana watu walichanga ili zigawanywe na si kuzikupatia na kufanyia shughuli zingine.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.