WAZIRI MWIJAGE AFUNGUA MAONESHO YA BIASHARA TANGA


Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha saruji cha Rhino Tanga, William Malonza, akimuonyesha moja ya bidhaa zizalishwazo na kiwanda hicho, Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, wakati wa maonyesho ya tano ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako Tanga. Mwijage ameyafungua maonyesho hayo leo katika viwanja ya maonyesho Mwahako ambayo yamezishirikisha mataifa mbalimbali ya Barani Afrika na Asia. 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akisalimiana na Afisa Masoko kiwanda cha saruji cha Rhino Tanga, Carolina Hillary wakati alipotembelea banda la maonyesho ya tano ya Kimataifa yalifunguliwa jana Tanga katika viwanja vya maonyesho Mwahako.
Waziri wa viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha Saruji cha Rhino Tanga, William Malonza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Tanga.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijaga akipata maelekezo ya namna mkonge unavyoweza kutengeneza dawa pamoja na mafuta aina mbalimbali.
Simba ni moja katika wanyama ambao wameletwa kwa ajili ya maonyesho Tanga.

Wakazi wa Tanga wakiangalia Kobe ambaye ni moja ya vivutio katika maonyesho ya tano ya Kimataifa yanayofanyika Tanga.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI