Yote aliyosema Meya wa Arusha baada tu ya kuachiwa na Polisi leo

Gumzo jingine la Arusha lilikua ni Meya wa Arusha, Madiwani, kiongozi wa Umoja wa wenye shule binafsi Arusha pamoja na viongozi wa dini kukamatwa na Polisi May 18 baada ya kufanya mkutano/kusanyiko kutoa rambirambi kwenye shule ya Lucy Vicent bila kibali.
Baada ya kuachiwa leo May 20 2017, Meya wa Arusha Kalist Lazaro ameongea na Waandishi wa habari na kusema >>> ‘Nilikamatwa nikiwa kwenye majukumu yangu ya kawaida kabisa kama Meya wa Jiji, majukumu ya kijamii kwenye shule ya Lucky Vicent ambayo hivi karibuni ilipoteza Wanafunzi 32 kwenye ajali’
‘Tarehe 16 mimi kama Meya wa Jiji nilipewa taarifa na umoja wa shule binafsi Tanzania (TAMOSCO) na NewLIFE ambayo ni NGO kutoka Ngaramtoni na baadhi ya watu wengine ambao walitaka kuhakikisha wanafikisha rambirambi zao kwa wafiwa’
‘Mimi ni Diwani wa Sokoni One, Wazazi waliofiwa wako 6 kwenye kata yangu, Diwani wa Olasiti ana familia 11 zilizofiwa… na Diwani mwingine Credo ana familia 6 zilizopoteza watoto, kwahiyo nikawaambia Madiwani wangu wahakikishe hizo familia zinakuwepo pale shuleni na mwenye shule akaandaa darasa moja ili tukio hilo lifanikiwe’
‘Moja ya vitu Wadau hao walitaka kuwe na maombi na nilimuandaa Padri wa Kanisa Katoliki, Mchungaji wa KKKT na kiongozi wa BAKWATA kutoka Olasiti, kabla ya zoezi la kukabidhi rambirambi mkononi kwa Wafiwa Polisi walivamia’
‘Mswali tulikua tunahojiwa ni kwanini fedha hizi hatujazipitisha kwa mkuu wa mkoa? nataka Watanzania wajue kwamba hakuna Kiongozi wa Serikali aliyefariki, walifiwa Wananchi wa kata zetu… mimi Meya wa jiji nimefiwa na Wananchi wangu’
‘Rambirambi za Wananchi zinatakiwa zipelekwe kwa waliofiwa na ndio maana siku nne zilizopita nilimtaka Mkuu wa mkoa aje hadharani awape rambirambi wale waliofiwa’ – Meya Kalist Lazaro
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI