BALOZI CISCO MTIRO KUZIKWA KESHO



Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro (pichani) ambaye amefariki dunia jana asubuhi  katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa siku ya JUMATANO, kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. Shaaban Kessy Mtambo

Mtambo ameiambia Globu ya Jamii kwamba mazishi ya mwanadiplomasia huyo yamepangwa kufanyika siku ya JUMATANO saa saba adhuhuri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 
Hiyo ni baada ya kuwasili watoto wake walioko Marekani ambao wanategemewa kuwasili Jumanne usiku, pamoja na mjane wa marehemu anayetegemewa kuwasili Jumanne mchana akitokea Bangui, Afrika ya Kati.
Amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nyumbani kwa marehemu saa tano asubuhi siku hiyo ya JUMATANO ambapo utafanyiwa kisomo na kuswaliwa kabla ya kuelekea makaburini kwa mazishi.
 Msiba upo nyumbani kwa marehemu mikocheni B jijini Dar es salaam ambako ndugu, jamaa marafiki, majirani na waliofanya kazi na marehemu wamekuwa wakimiminika kutoa mkono wa pole kutwa nzima ya jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huu.

Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi - AMINA

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.