Breaking News: Polisi Dar Waua Watuhumiwa Wawili wa Ujambazi, Mmoja Ajeruhiwa


JESHI LA POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaua watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi huku mmoja akijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

Akitoa ripoti ya mafanikio ya Jeshi hilo, Kamanda wa Operesheni, ambaye pia ni Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amesema kuwa jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata silaha mbili na risasi 5.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar, mnamo 19/06/2017 majira ya saa saa 1:30 jioni maeneo ya Kigogo Luhanga lilifanikiwa kukamata majambazi wawili wakiwa na shotgun na risasi 5 baada ya majibizano ya risasi kati ya majambazi hao.

“Wakiwa katika doria, askari waliona pikipiki mbili za wa zilizobeba watu wawili wawili kila moja, polisi walizifuatilia baada ya kuwatilia shaka watu hao. Watu hao walibaini kuwa wanafuatiliwa kuwa wanafuatiliwa na kuanza kurisha risasi ambapo wawili walijeruhiwa. Baada ya uchunguzi ilibainika ni majambazi waliofanya mauaji maeneo ya Makuburi huku wenzao wawili wakikimbia na pikipiki.

“Katika harakati za kuwapeleka hospitali majambazi waliojeruhiwa, walifariki dunia wakiwa njiani,” Alisema Mkondya.
MSIKIE KAMANDA AKIZUNGUMZA
Tupia Comment Yako, Matusi Hapana
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

ZAKIA MEGHJI AWATIA HAMASA GIRL GUIDES, ATAKA WAWE JASIRI

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)