BULEMBO AMALIZA ZIARA KATIKA WILYA 47 ZA MIKOA SABA, JOTO LAKE LASABABISHA CHADEMA 376 KUTIMKIA CCM


Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisiriki kuapa wakati wanachama wapya waliohamia CCM kutoka Chadema walipokuwa wakiapa na kuungwa mkono na wanachama wote katika kiapo hicho
Wanachama wapya wa CCM wakiapa
Wanachama wa CCM wapya wakiapa huku wakiungwa mkono na wanachama wote waliokuwa ukumbini, kula kiapo hicho
Alhaj Bulembo akimvalisha kofia mmoja wa wanachama hao wapya
Alhaj Bulembo akiwahoji baadhi ya madiwani kuhusu mahusiano yao ya karibu na mabalozi yalivyo
Alhaj Abdallah Bulembo akiwa tayari kikabidhi kwa diwani fedha zilizochangwa kwa ajili ya kumsaidia mlemavu mmoja aliyeomba msada wakati wa kikao hicho
Alhaj Bulembo akikabidhiwa zawadi mwishoni mwa kikao hicho
Alhaj Bulembo akiagana na baadhi ya wanachama wakati akitoka ukumbini baada ya kikao hicho mjini Geita.
Alhaj Bulembo akiwa katika Kivuko cha mv Sabasaba tayari kwa safari ya kwenda Mwanza jioni.
Baadhi ya wandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara wa Alhaj Bulembo wakiwa ndani ya Kivuko hicho
Alhaj Bulembo akiwa ameketi na kiongozi mmoja wa CCM katika kivuko hicho

Alhaj Bulembo akizungumza jambo na Doto wakiwa kwenye Kivuko hicho

Alhaj Bulembo akitoka kwenye Kivuko hicho mwishoni mwa safari. PICHA: BASHIR NKOROMO
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdalah Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mbogwemkoani Geita, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za CCM, Mbalozi na Watendaji wa Serikali katika Wilaya hiyo, jana, Juni 10, 2017.
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipokea kadi kutoka kwa mmoja wa wanachama sita wa Chadema, waliotangaza kutahmia CCM wakati wa kikao hicho.
Stephen Thobias akizungumza baada ya kutangaza kuachana na Chadema na kujiunga na CCM wakati wa kikao hicho
Nyambina Chacha akizungumza baada ya kutangaza kukihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa kikao hicho
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akionyesha kadi za Chadema baada ya waliokuwa wanachama wa chama hicho kumkabidhi na kuhamia CCM wakati wa kikao hicho. Waliosimama mbele ni wanachama hao baada ya kukabidhiwa kadi za CCM
GEITA🔽
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCm Alhaj Abdallah Bulembo akivishwa skavu baada ya kuwasili ofisi ya CCM wilaya ya Geita mkoani Geita, jana.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akienda ukumbini baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Geita mkoani Geita, jana
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiingia ukumbini huku akishangiliwa kwa nderemo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili meza kuu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzani, mkoa wa Geita, Mbunge wa Bukombe Doto Biteko na kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Wilaya ya Geita Ahmed Mbaraka na Katibu wa CCM Wilaya ya Geita Muhoja mapande
Alhaj Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuketi ukumbini
Mwenyekiti wa umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Geita AllyRajabu kihamasisha wakati akisaliia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wakiwa ukumbini
Na Bashir Nkoromo

Hatimaye Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi na Mbunge wa Kuteulia na Rais Alhaj Abdallah Bulembo, amemaliza ziara yake ya Kichama akiwa amefanikiwa kutembelea mikoa saba na jumla ya Wilaya 47 za mikoa hiyo.

Katika ziara hiyo ambayo alianza May 26, 2017, aliihitimisha jana, Juni 10, 2017 katika mkoa wa Geita, ziara ikiwa imechukua zaidi ya wiki mbili, ambapo mkoa wa kwanza kufanya ziara hizo uliuwa Dar es Salam na badaye kuendelea katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Tabora, Kigoma, Kagera na Geita ambao ndio mkoa aliomalizia.

Alhaj Bulembo katika ziara hiyo ambayo haikuhusu Jumuia yake ya Wazazi Tanzania, bali ya Kichama zaidi ilikuwa mahsusi kwa kuagizwa na Bosi wake, Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli, kwa lengo la kutoa shukrani kwa wana CCM kufuatia kura nyingi walizompa hadi kukipatia Chama Cha Mapinduzi kura nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2015.

Hata hivyo Bulembo anasema, Shukrani hizo, ni za awali kwa kuwa Mwenyekiti Mwenyewe Rais Dk. John Magufuli atafanya ziara rasmi kutoa shukrani.

Katika ziara hiyo, Alhaj Bulembo pia pamoja na mambo mengine ya kuhimiza ujenzi na uimarishaji Chama na Jumuia zake, alikuwa na ajenda za kufafanua kuhusu mabadiliko yaliyowaacha nje badhi ya waliokuwa Mabalozi na pia kufafanua kwa kina umuhimu wa Mabalozi wapya waliopatikana sasa na wale waliobaki kutokana na mabadiliko hayo ndani ya Chama.

Alhaj Bulembo kwenye vikao vya ndani kwenye ziara hiyo alipata fursa za kuwapiga msasa, kwa kuwapa darasa zito Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM katika Wilaya husika, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia zote za Chama, Mabalozi na Watendaji wote wa serikali.

Mara kadhaa alisisitiza umuhimu wa madiwani kuwa karibu na viongozi wa Chama hasa mabalozi, ikiwa ni pamoja na kuwatambua kwa karibu hadi kwa majina na kujenga mahusiano ya kawaida kwa lengo la kukuza ukaribu baina yao na viongozi hao, siyo tu wa kichama bali hadi wa kifamilia.

Katika hali ambayo haikuwa ikitarajiwa, katika wilaya karibu zote alizofika, ilionekana dhahiri kwamba madiwani karibu wote walikuwa hawana mahusiano ya kawaida na mabalozi, hali hii ilijidhihirisha pale Alhaj Bulembo alipokuwa akiwasimamisha madiwani na kumuuliza kila mmoja alivyoshiriki kwenye uchaguzi wa mabalozi, idadi ya mashina na majina ya mabalozi katika kata zao.

Madiwani wengi walijikuta wengine hawajui hata idadiya mashina katika kata zao, na pia walishindwa kutaja idadi ya mabalozi kwenye eneo lao, na kutaja majina ya mabalozi ndiyo ilikuwa kazi kubwa. Diwani alijikuta akitaja balozi mmoja au wawili tu, kata nzima.

"Mnajua lengo la mahusiano haya, ni kukirahisisha Chama kupata kura kwa urahisi wakati wa uchaguzi, kwa sababu ninyi madiwani mkiwa mmeshajenga mahusiano na Wenyeviti wenu wa mitaa na mabalozi hakutakuwa na kazi ngumu ya kutafuta kura, na lazima mtambue kuwa Mabalozi ndiyo siri kubwa ambayo hufanikisha ushindi wa CCM katika chaguzi", anasema Bulembo kwa nyakati tofauti.

Mbali na darasa alilokuwa akitoa kwenye vikao hivyo, katika ziara hiyo amewesha CCM kujizolea wanachama wapya 376 ambao walikihama chama cha Chadema na kujiunga na CCM, wakiwemo waliokuwa viongozi wa Chadema katika vitongoji na Vijiji na aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Baada ya Makala hiyo fupi yafuatayo ni matukio katika picha katika ziara ya mwisho wa ziara hiyo ambayo Bulembo aliifanya jana katika Wilaya za Mbogwe na Geita mkoani Geita.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI