4x4

Dogo Janja Munalove Kulikoni?


Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ .
STAA wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ anadaiwa kulelewa na mwanamama ambaye ni msanii wa filamu wa zamani, Muna Alphonce ‘Munalove’ na sasa wanapika na kupakua.
Msanii wa filamu wa zamani, Muna Alphonce ‘Munalove’.
Chanzo makini kiliiambia Risasi Vibes kuwa, wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja mara nyingi ambapo ukaribu huo unaonesha kwamba ni wapenzi na inasemekana mwanamama huyo ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mwanamuziki Kalala Junior ndiye anayemfanya msanii huyo kuonekana akipigilia nguo za thamani tofauti na zamani.

   Muna Alphonce ‘Munalove’.
Baada ya kupata habari hizo, Risasi Vibes iliwatafuta wawili hao ambapo majibu yao yalionesha kujichanganya na kuzua sintofahamu zaidi kwani Dogo Janja alikanusha kwamba siyo kweli na hamfahamu kabisa mwanamama huyo.
Upande wa Muna alisema; “Dogo Janja ni mdogo wangu sana na ninamchukulia hivyo siyo mpenzi wangu jamani.”
Post a Comment